Baada
ya kupagawisha wananchi wa Mbeya na shoo kali mwishoni mwa wiki iliyopita,
tamasha la Serengeti Fiesta 2014 linaelekea Singida kukata kiu ya mashabiki wake
ambao walikuwa wakilisubiri kwa hamu.
Shoo
hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu imepangwa kufanyika hapo Septemba 3, katika
uwanja wa Namfua. Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake namba moja
cha Serengeti Premium Lager ambao ndio wadhamini wa tamasha hilo wamejipanga
kutoa shoo bora kabisa kwa wananchi wa mkoa wa Singida.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Meneja Chapa wa Kiwanda cha Serengeti Bwana Rugambo
Rodney alidhibitisha uwepo wa wasanii watakaoporomosha shoo kali siku hiyo kuwa
ni pamoja na Mwana Fa, Nikki II, Makomando, Stamina, Ney, Young Killa, Linah,
Recho, Mr. Blue, Dully Sykes, Mo Music, Baraka Da Prince, Supa Nyotas:-
(G-Luck, K-Style na Edo boy), “ Rodney aliendelea kusema kwamba....”Wakati
ziara hiyo ikielekea ukingoni, ahadi yetu kwa mashabiki wetu wa Iringa ni
kujiweka tayari kwa shoo kali hapo mjini kwao.”
Mwana Fa ambaye atatumbiza kwa mara ya
kwanza katika shoo za tamasha la Serengeti Fiesta mjini Singida mwaka huu
alisema....”Nimefarijika kuwa mmoja wa wasanii watakaotumbuiza mjini Singida na
ningependa kuwashauri mashabiki wangu waje kwa wingi kunishuhudia jukwaani
nikifanya mambo wakati wa shoo.”
Kabla ya
shoo hiyo, kutakuwa na shughuli nyingine mbalimbali kama shindano la Serengeti
Super Nyota Diva ambalo mshindi atajinyakulia tiketi kwenda kushuhudia shoo ya
mwisho ya tamasha hilo litakayofanyika hapo Oktoba 18, 2014 jijini Dar Es
Salaam.
No comments:
Post a Comment