Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 27 October 2014

SAMANTHA POWER ATAKA MATAIFA YAWAJIBIKE

Samantha Power, Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa.
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa ameanza ziara ya kuzitembelea nchi tatu zilizoathirika zaidi na mlipuko wa Ebola, akikosoa msaada wa kimataifa katika kukabiliana na ugonjwa huu.

Samantha Power ametua Guinea na atatembelea Sierra Leone na Liberia.
Ameliambia shirika la Utangazaji la Marekani, NBC kuwa baadhi ya mataifa ambayo yaliahidi msaada "bado hayajawajibika" katika kutoa msaada na madaktari.
Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani za hivi karibuni, zaidi ya watu 10,000 wameambukizwa virusi vya Ebola, huku watu 4,922 wakipoteza maisha.
Wafanyakazi wa afya wanaowahudumia wagonjwa wa Ebola
Wagonjwa hawa ni kutoka nchi za Sierra Leone, Liberia na Guinea, isipokuwa 27 kati yao.
Bi Power ameiambia NBC wakati akipanda ndege yake yenye maandishi: "Mwitikio wa kimataifa kuhusu Ebola unatakiwa kuchukuliwa kwa namna tofauti kabisa kuliko ilivyo sasa hivi."
Amesema: "Mna nchi katika Umoja wa Mataifa ambako nafanyakazi kila siku watu ambao wanatia saini maazimio na kusifia kazi nzuri ya Marekani na Uingereza na nyinginezo, lakini wenyewe hawajachukua hatua zozote za kuwajibika kwa kuwatuma madaktari, kutuma vitanda, na kutoa kiasi cha fedha kinachofaa."
Samantha Power amekuwa mkosoaji kuhusu mwitikio wa kimataifa katika kukabiliana na ugonjwa wa Ebola.
Atatembelea vituo vya kitaifa vya kuratibu shughuli za kukabiliana na Ebola na kukutana na wafanyakazi wa Marekani na Umoja wa Mataifa, ingawaje haikuwekwa wazi kama atakutana na watu walionusurika kifo baada ya kuugua Ebola.
Marekani imeahidi wanajeshi 4,000 kujenga hospitali na kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa afya, Afrika Magharibi, ambapo askari 600 tayari wamewasili huko.
CREDIT: BBC/SWAHILI

No comments:

Post a Comment