Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 30 October 2014

AINA MPYA 27 ZA WANYAMA ZAGUNDULIKA TANZANIA

Na Florence Majani, Mwananchi
Profesa Neil Burgess, anayeongoza barani Afrika kwa utaalamu wa baioanuai na mwenyekiti mwenza wa TFCG, anasema milima ya tao la Mashariki imekuwa ikijulikana kwa muda mrefu kuwa na aina nyingi za viumbe ijapokuwa kumekuwa na ukosefu wa takwimu sahihi hasa katika maeneo sita kati ya 13 ya milima hiyo.
Charles Leonard wa TFCG anasema uwepo wa misitu hiyo kwa mamilioni ya miaka umechangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa aina tofauti za viumbe hai.
“Utafiti huu unaonyesha umuhimu wa kuitunza zaidi misitu hii.  Misitu hii ya Tao la Mashariki imetengwa katika mnyororo wa kijiolojia wa kizamani wenye maeneo 13 yanayoanzia kusini mwa Kenya hadi kusini na kati nchini Tanzania,” anasema.
Changamoto
Meneja mradi wa misitu wa TFCG, Elinasi Monga anasema kwa sasa kuna changamoto kubwa katika misitu ikiwa ni pamoja na ongezeko la watu na kazi zao kama vile kilimo, biashara ya mbao na ujenzi.
Licha ya umuhimu wake kibaiolojia, ukataji na uharibifu wa misitu unaendelea kuuathiri.
Utafiti uliofanywa na taasisi za Mjumita na TFCG umebaini kukatwa kwa hekta 100 za miti kila mwaka katika misitu ya asili ya Mkingu Kusini mwa milima ya Nguru kati ya mwaka 2010 na 2014.
Monga anasema faida ya misitu hiyo siyo kuwaruhusu wananchi kuikata bali ni kwa dunia nzima kwa kupata maji na kukuza uchumi kwa utalii.
“Faida ya misitu siyo kuwaruhusu wananchi kwenda kukata miti, ni ulimwengu mzima. Tuombe kuingia kwenye urithi wa dunia ili tudai hata fidia kwa ajili ya wananchi wetu,” anasema Monga.
“Leo tunashindwa kuzalisha umeme kwa sababu ya upungufu wa maji, tunakosa maji ya kutumia kwa sababu ya uharibifu wa misitu,” anasema Monga.
Anasema sababu hasa ya kuharibu misitu haitaishia Tanzania tu bali itakuwa kwa dunia nzima hivyo akasisitiza umuhimu wa jumuiya ya kimataifa kuchangia utunzaji wa misitu hiyo.
Mkurugenzi mtendaji wa TFCG, Charles Meshack anasema suluhisho la yote hayo ni kuomba Shirika la Elimu na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (Unesco) ili misitu hiyo ingizwe kwenye urithi wa dunia.
“Tunaishauri Serikali iutumie utafiti huu kama msingi wa kuifufua misitu yetu na kuomba Unesco iingizwe kwenye maeneo ya urithi wa dunia ili uangaliwe kwa makini na jumuiya ya kimataifa,” anasema Meshack.
Meshack anasema kulikuwa na mchakato huo tangu mwaka 2005 hadi hadi ulipoachwa na Rais Jakaya Kikwete mwaka 2011.
“Mwaka 2011 Rais Kikwete aliagiza kuwa misitu ya tao la Mashariki uondolewe kwenye mchakato wa kuingizwa kwenye urithi wa dunia unaofanywa na Shirika la Elimu na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (Unesco),” anasema Meshack.
“Yalikuwa ni mambo ya kisiasa tu kwa sababu wakati huo Serikali ilikuwa ikiomba eneo la pori la akiba la Selous litolewe kwenye urithi wa dunia ili lichimbwe madini ya urani.
“Tunamwomba Rais Kikwete arudishe mchakato huu kwani kuna faida kubwa,” anasema.
Akifafanua kuhusu suala hilo, mkurugenzi mwandamizi katika Wizara ya Maliasili na Utalii, Lawrence Mbwambo amekiri kusitishwa kwa mchakato huo na kusema kuwa umeanzishwa upya, lakini utachukua muda mrefu.
Misitu ya tao la Mashariki
Misitu ya Tao la Mashariki imesaidia kutunza vyanzo vya maji yanayotiririka katika mito mikubwa kama vile Ruvu, Rufiji, Wami, Pangani na Zigi.
“Kati ya viumbe aina 23 ya 27 zilizogunduliwa, kuna amfibia na reptilia. Baadhi yao wameishi hadi miaka 100 milioni na ni ushahidi wa umri mrefu, uimara na upekee wa historia ya milima hiyo,” anasema mtafiti, Michele Menegon.
Misitu hiyo inaanzia milima ya Taita nchini Kenya na kuingia nchini Tanzania kupitia milima ya  Upare Kaskazini na Kusini, Usambara Magharibi na Mashariki, Nguu, Nguru, Uluguru, Ukaguru, Rubeho, Malundwe, Udzungwa na Mahenge. Anasema kugundulika kwa viumbe hao kunaweza kusaidia kukuza utalii nchini.

CREDIT: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment