Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday, 27 October 2014

KANISA LACHANGANYA UDONGO WA ISRAEL NA TANZANIA ILI KUITABIRIA NCHI MAFANIKIO


Na Mwandishi Wetu, BrotherDanny Blog
Arusha:
UONGOZI I wa kanisa la Lift Him Up lililopo maeneo ya Sanawari jijini hapa limeuchanganya udongo wa nchi ya Israel pamoja na wa Tanzania kwa makusudio kuwa Tanzania inatakiwa kuwa moja ya nchi zenye kujivunia rasilamali zake tofauti na sasa ambapo asilimia kubwa ya rasilimali haziwanufaishi hata kidogo Watanzania.



Pia uchanganywaji wa udongo huo ni ishara ya kuombaamani katika nchi ya Tanzania hususani kwa nyakati kama hizi ambapo taifa lina mchakato wa uchaguzi mkuu lakini pia hata katiba mpya.

Akiongea katika zoezi hilo la uchanganyaji wa udogo mgeni rasmi ambaye ni Askofu Aminiel Mgonja alisema kuwa maonio ya kuchanganya udongo nak,isha kuomba kwa mungu nchi ibarikiwe yalitokea kwa mchungaji kiongozi wa kanisa la Lift him ambaye ni Ockaye Mgonja.

Askofu huyo alidai kuwa kitendo hicho ni moja ya kitendo cha imani sana na kitaweza kufanya mabadilko makubwa sana hapa nchini huku mabadiliko hayo yakiwa ni moja ya malengo au makusudio ya kuchukua udongo huo.

Alidai kuwa nchi ya Tanzania imebarikiwa sana katika rasilimali mbalimbali lakini kitu cha ajabu ni kuwa rasilimali hizo bado hazijaweza kuwanufaisha watanzania wenyewe jambo ambalo sio makusudio kabisa ya Mungu kwa nchi hii.

"tujiulize kuwa hii nchi ina vitu vingapiambavyo kama vingetumika vema basi vingeweza kuwasaidia watanzania wenyewe na jekwanini tuwe tegemezi kwenye mataifa mengine wakati uwezo wa kupiga hatua sisi kama sisi tunao lazima tukatae hii hali"aliongeza Askofu huyo.

Naye mchungaji kiongozi wa kanisa hilo,Ockey Mgonja alisema kuwa amepata maono makubwa sana ya kuweza kulifanya taifa la Tanzania libadilike na kuwa miongoni mwa mataifa yenye utajiri mkubwa sana duniani tofauti na sasa ambapo rasilimali zipo lakini zinashindwa kutumika ipasavyo.

No comments:

Post a Comment