Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 30 October 2014

HII SASA KALI: MUME MKOROFI AANDALIWA MLO WA KONDOMU!

Kondomu
Mwanamke mmoja mwenye watoto watatu katika wilaya ya kole nchini Uganda alimuandalia mumewe mlo wa mipira ya kondomu kufuatia ugomvi usiokwisha.

Mwanamke huyo ambaye ni mkaazi wa eneo la Arao aliripotiwa kununua paketi tatu za kondomu aina ya Trust kutoka duka jirani kabla ya kuzipika na kumuandalia mumewe kama chakula baada ya kurudi nyumbani akiwa amelewa chakari.
kulingana na gazeti la bdaily monitor nchini Uganda inadaiwa kuwa mwanamke huyo aliikata kata mipira hiyo ya kondomu ambayo ilikuwa haijatumika katika vipande vidogo vidogo na kuvichemsha kwa mda kabla ya kuvikaranga na mafuta ya kupikia na viungo vyenginevyo.
Wakati mumewe alipowasili kutoka kubugia pombe katika eneo jirani la kibiashara la Odede,aliandaliwa mlo huo katika sahani tofauti moja ikiwa na mipira hiyo kama mboga na nyengine ikiwa na makaa.
Lakini jamaa huyo alibaini njama za mkewe baada ya kuonja mlo huo na kugundua ulikuwa na ladha tofauti.
Hatua hiyo ilikuwa ikilenga kumfunza mume huyo ambaye amedaiwa kuzua ugomvi na mkewe kila anapolewa na kurudi nyumbani.
CREDIT: BBC/SWAHILI

No comments:

Post a Comment