Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday, 31 October 2014

UFISADI WA BILIONI 3.2/- WABAINIKA TWIGA BANKCORP


Mwenyekiti wa PAC, Deo Filikunjombe

Na Isaya Kisimbilu
Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), imeibua ufisadi wa zaidi ya Sh. bilioni 3.2 katika Benki ya Twiga Bancorp, kutokana na wizi unaodaiwa kufanywa na baadhi ya wafanyakazi wa taasisi hiyo ya fedha kwa muda mrefu.

Ufisadi huo ulibainishwa na ofisi ya CAG kwenye kikao  baina ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya  Hesabu za Serikali (PAC) na uongozi wa benki hiyo jana.

Makamu Mwenyekiti wa PAC, Deo Filikunjombe (pichani), alisema, ripoti hiyo ya CAG inaonyesha kuwa, kiasi hicho cha fedha ambazo ni za wateja, zimekuwa zikiibwa kwa muda mrefu tangu kuanzishwa kwa tawi  la benki hiyo la Mlimani City mwaka 2004.
Ufisadi huo unajumuisha pia Sh. milioni 540 ambazo katika vitabu vya mahesabu vya benki hiyo vinaonyesha zinadaiwa na watu wasiojulikana, huku nyingine zikionekana kutengwa kwa ajili ya kushughulikia masuala ya bima ambazo hata hivyo hazikutumika kama ilivyokusudiwa.
Aidha, katika ukaguzi wake kwa benki hiyo, ofisi ya CAG ilipotaka kutajiwa majina ya watu wanaodai kiasi hicho cha fedha ili wajulikane na kisha kuingizwa kwenye taarifa yake (CAG), uongozi wa benki hiyo haukuweza kufanya hivyo.
Filikunjombe aliuhoji uongozi wa bodi hiyo kueleza aina ya hati waliyopewa na CAG, sababu zilizonyuma ya kupewa hati ya namna hiyo na kueleza iwapo wanaifurahia hali hiyo.
Mwenyekiti wa bodi ya taasisi hiyo, Profesa Amon Mbelle, alisema benki  ilipokea hati yenye mashaka kutoka ofisi ya CAG kutokana na matatizo mbalimbali likiwamo la usimamizi mbovu wa uongozi.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment