Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 31 October 2014

RAIS COMPAORE AJIUZULU, JESHI LASHIKA HATAMU BURKINA FASO

Bwana Compoare amejiuzulu
Aliyekuwa rais wa Burkina Faso Bwana Compaore sasa ametaka uchaguzi mpya wa urais ufanyike baada ya siku 90.

Hata hivyo hakubaini ikiwa afisa huyo wa kijeshi alikuwa akizungumza kwa niaba ya jeshi lote.
Jeshi lilisema kuwa litafanya mkutano na waandishi habari.
Maelfu ya waandamanji walikuwa wamerejea mabarabarani kwa siku ya pili
Siku ya alhamisi waandamanaji waliokuwa wamekasirishwa na jitihada za rais za kuongeza muda wa uongozi wake wa miaka 27 walitetekeza bunge na kuvamia kituo cha runinga ya taifa.
Bwana Compaore alitupilia mbali jitihada za kubadilisha katiba ambayo ingemruhusu kuwania tena muhula mwingine kama rais lakini akasema kuwa angebaki madarakani kwa mwaka moja zaidi .
Awali, Msemaji wa Jeshi amewaambia waandishi wa habari mjini Ouagadougou kuwa bwana Compaore hayuko mamlakani tena.
Rais Compaore alikuwa ametangaza kuwa atajiuzulu baada ya kipindi cha serikali ya mpwito ya mwaka mmoja .
Lakini wanasiasa wa upinzani wakakataa kata kat kuendelea kwa utawala wake na wakamtaka ajiuzulu maramoja.
Rais Compaore alikuwa ameongoza kwa zaidi ya miaka 27 tayari.
Kumeripotiwa maandamano mapya nchini Burkina Faso ya kutaka kujiuzulu mara moja kwa rais wa nchi hiyo Blaise Compaore.
Viongozi wa upinzani wanakutana kwenye mkji mkuu Ouagadougou kukubaliana kwa pamoja hatua watakazochukua.
Siku ya Alhamisi waandanamaji walikarisishwa na jitihada za rais za kuongeza kipindi chake chake miaka 27 madarakani na wakateketeza bunge na kusaka kituo cha runinga cha serikali.
Rais Compaore ametangaza kuvunjwa kwa serikali na bunge
Bwana Compaore alitupilia mbali jitihada za kubadilisha katiba ambayo ingemruhusu kuwania tena muhula mwingine kama rais lakini akasema kuwa atabaki madarakani kwa mwaka moja zaidi .
Viongozi wa Upinzani Nchini Burkina Faso wamewaomba waandamanaji kutolegeza kamba bali kuendelea na maandamano huku wakimtaka Rais Blaise Campaore ang'atuke mamlakani mara moja.
Licha ya Rais Compaore wa Burkina Faso kuhutubia taifa siku moja baada ya vurugu kubwa na kutangaza kuvunja serikali waandamanaji hawataki kusikia kwamba apewe muda wa mwaka mmoja ndipo aondoke madarakani.
Jana jioni kiongozi wa Jeshi Jeneral Honore Traore alitangaza kuundwa kwa serikali ya mpwito itakayodumu kwa kipindi cha mwaka mmoja japo hakusema ninani atakayeiongoza.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment