Mfanyakazi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Bi.
Mariam Tambwe akimkaribisha mgeni rasmi ambaye pia ni Mkuu wa Chuo hicho kwa
ajili ya kufanya ufunguzi rasmi wa mafun z ohayo na kutowapa wajasiriamali
maneno ya busara katika mafunzo ya siku mbili (24-25 Oktoba, 2014) chuoni hapo
ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho
jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) cha jijini
Dar es Salaam, Profesa Emmanuel Mjema akifungua rasmi mafunzo maalum kwa
Wajasiriamali (hawako pichani) walioko katika mafunzo ya siku mbili (24-25
Oktoba, 2014) chuo hapo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 tangu
kuanzishwa kwa chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Mwezeshaji wa mafunzo ya Ujasiriamali wa Chuo cha
Elimu ya Biashara (CBE), Bw. Ndingo Mwakyusa akiwapa elimu wajasiriamali
waliohudhuria mafunzo ya siku mbili (24-25 Oktoba, 2014) chuoni hapo ikiwa ni
sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho jijini Dar es
Salaam.
Mwezeshaji wa mafunzo ya Ujasiriamali wa Chuo cha
Elimu ya Biashara (CBE), Bi. Suma Nelson Mwansasu akiwapa elimu wajasiriamali
waliohudhuria mafunzo ya siku mbili (24-25 Oktoba, 2014) chuoni hapo ikiwa ni
sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho jijini Dar es
Salaam.
Baadhi ya Wajasiriamali waliohudhuria mafunzo ya
siku mbili (24-25 Oktoba, 2014)wakifuatilia kwa makini elimu ikiyotolewa katika
mafunzo hayo chuoni hapo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 tangu
kuanzishwa kwa chuo hicho jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE
NA BENEDICT LIWENGA, MAELEZO-DSM)
Na Benedict Liwenga, Maelezo-DSM
CHUO cha Elimu ya Biashara (CBE) cha jijini Dar es Salaam kimefungua rasmi Mafunzo ya siku mbili ya Ujasiriamali kwa Wajasiriamali wa jijini Dar es Salaam ikiwa ni moja ya sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho.
Akifungua rasmi mafunzo hayo leo 24 Oktoba mwaka huu, Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Emmanuel Mjema amesema kuwa, mafunzo hayo kwa wajasiriamali hao itakuwa chachu ya maendeleo kwani yanalenga kutoa elimu ya biashara ili waweze kukokotoa mahesabu na kuongeza faida katika na shughuli zao za kijasiriamali.
Profesa Mjema Ameeleza kuwa, ujasiriamali nchini ni sekta muhimu kwani zaidi ya asilimia 85% ya waajiriwa nchini wanatoka katika sekta hiyo, huku asilimia 15% ni ya watumishi wa umma.
Amefafanua kuwa, mjasiriamali ni mtu yule ambaye amethubutu kwa kuwekeza rasilimali zake ili aweze kuendeleza kipato chake mwenyewe na kwa kufanya hivyo, anapunguza tatizo la ukosefu wa ajira nchini ambalo limekuwa ni tatizo linalowakabili wajasiriamali wengi.
“Nawapongeza sana kwa kazi nzuri mnazozifanya za ujasiriamali, hakika mchango wenu ni mkubwa kwa jamii nchini na unasaidia kupunguza tatizo la ajira nchini mwetu”, alisema Profesa Mjema.
Aidha, amewaasa wajasiriamali hao kuzingatia mafunzo hayo kwa kuhakikisha kuwa wanatunza faida na kuweza kukokotoa mahesabu vizuri huku akibainisha kuwa, tatizo linalowakumba baadhi ya wajasiriamali nchini sio tu mtaji, bali ni elimu ya kibiashara ambayo inawawezesha kufanya shughuli hiyo na kupata faida, hivyo amewataka kuzingatia mafunzo hayo na kuyatumia kivitendo katika kuleta maendeleo yao wenyewe na kwa taifa kwa ujumla.
“Tafiti zinaonyesha kuwa, wajasiriamali wengi wanaanguka katika biashara zao kwa kukosa elimu ya biashara”, aliongeza Profesa Mjema.
Sambamba na mafunzo hayo, chuo hicho kinatarajia kutoa huduma ya vifaa mbalimbali vya hospitalini ikiwa ni sehemu ya mchango wake wa kuisaidia jamii.
Nao wawezeshaji wa mafunzo hayo ya ujasiriamali akiwemo Bwana Ndingo Mwakyusa pamoja na Bi. Suma Mwansasu wamesema kuwa mafunzo hayo wanayoyatoa kwa wajasiriamali hao yanahusisha elimu ya biashara ikiwemo mada mbalimbali kwa wajasiriamali hao kuhusu umuhimu wa ujuzi wa ujasiriamali katika ulimwengu wa kibiashara, kutengeneza hulka za kijasiriamali, vigezo muhimu vya kuzingatia katika biashara, vigezo muhimu katika uendeshaji wa biashara na mengineyo.
Mafunzo hayo ya ujasiriamali yanatarajiwa kuendelezwa kwa baadhi ya mikoa ya Pwani, Mbeya, Dodoma, Mwanza pamoja na upande wa Zanzibar.
No comments:
Post a Comment