Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 27 October 2014

KARIATI YAKABIDHI MATREKTA MANNE KWA WAKULIMA WA KONDOA NA MBARALI

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kariati Matrekta, Alhaji Omari Kariati akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), wakati wa hafla ya kukabidhi matrekta hayo jijini Dar es Salaam juzi.
 Mmoja wa wakulima, Khalifa Huruvi  kutoka Kijiji cha Kwadelo Kondoa mkoani Dodoma akitoa maelezo yake baada ya kukabidhiwa trekta.
 Mkulima Sengeri Bakari naye akitoa maelezo yake baada ya kukabidhiwa trekta lake.
 Matrekta waliyokabidhiwa yanavyoonekana 
baada ya kuunganishwa.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kariati Matrekta, Alhaji Omari Kariati (kushoto), akifurahi wakati akijaribu moja ya matrekta hayo kabla ya kuwakabidhi wakulima hao. Kulia  ni mkulima Karoli Lubuva.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kariati Matrekta, Alhaji Omari Kariati (kushoto), akikata utepe kuashiria makabidhiano hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kariati Matrekta, Alhaji Omari Kariati, akimkabidhi funguo wa trekta, Mkulima Karoli Lubuva katika hafla hiyo. Wengine wanaoshuhudia tukio hilo ni wakulima kutoka Kwadelo mkoani Dodoma.

Na Mwandishi wetu


KAMPUNI ya Kariati Trekta imewakabidhi matrekta manne yenye thamani ya Shs. 100 milioni kwa wakulima kutoka mkoani Mbeya na wilayani Kondoa baada ya kuwakopesha kwa bei nafuu.


Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kukabidhi matrekta hayo jijini Dar es Salaam juzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kariati Matrekta, Alhaji Omari Kariati alisema matrekta hayo yatawasaidia katika kilimo ambacho kitawainua kiuchumi.


Alisema kampuni hiyo kwa kipindi cha miaka miwili imewakopesha wakulima zaidi ya matrekta 84 ambapo kila anayekopa anatakiwa sh.milioni 25 kwa awamu mbili.


"Kila mkulima anaye kopeshwa kwa awamu ya kwanza anatakiwa kutoa sh.milioni 18 na baadae anamalizia kiasi kilichobaki" alisema Kariati.


Alisema kampuni yake hiyo imelenga kuwasaidia wakulima kuepukana na jembe la mkono na linatoa mkopo huo kwa mkulima yeyote ndani ya Tanzania.


Kariati alitoa mwito kwa wakulima kutumia fursa hiyo ya kukopa matrektra hayo ili kujikomboa kiuchumi na kustawisha maisha yao na kuondokana na umaskini.(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)

No comments:

Post a Comment