Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 30 October 2014

JELA MWAKA MMOJA KWA KUMUOA BINTIYE WA MIAKA 11!

Waliobahatika kuwa shule ndo hao, wengine huanza shule ya awali wakiwa na miaka 11.
Wakati harakati mbali mbali za kukabiliana na ndoa na mimba za utotoni zikiendelea na hasa katika nchi za Afrika, baadhi ya nchi barani humo zinakabiliwa na changamoto hiyo kupita kiasi.

Ama kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni. Kesi ya kwanza na ya aina yake imefanyika na hukumu yake kutolewa nchini Ivory Coast baada ya mwanamume mmoja kumuoa binti yake wa umri wa miaka 11.
Kutokana na kitendo cha mwanamume huyo kumuoa binti yake alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela na faini ya dola za Kimarekani 700.
Mwendesha mashtaka Rosine Kone amesema kwamba kesi hiyo ya aina yake itatuma ujumbe mzito kwa raia wa nchi hiyo ili wanaume waache tamaa.
Nao Umoja wa Mataifa unasema kwamba ndoa za utotoni nchini Ivory Coast si suala la kushangaza, kwani mmoja kati ya mabinti watatu huolewa kabla ya kufikisha umri wa miaka 18.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment