Mr Blue atafanya vitu vyake ndani ya Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma
Shoo ya tamasha la Serengeti Fiesta 2014
limeelekea Kigoma leo tarehe Oktoba 25, baada ya kuburudisha vilivyo jijini Dar
es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo zaidi ya mashabiki 50,000
walihudhuria katika tamasha hilo.
Tamasha
la Serengeti Fiesta limeingia mjini Kigoma, kama sehemu ya kuwapa zawadi mashabiki wake kutokana na mafanikio makubwa
waliyowahi kuyapata mkoani humo. Shoo hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa
na mashabiki wa mkoa huo imepangwa kufanyika katika uwanja wa Lake Tangayika
ambapo wakazi wa mji huo wanahamu kubwa ya kuona wasanii nyota wakituimbuiza kwa mara ya kwanza katika
mkoa huo.
Kwa
mujibu wa taarifa toka kiwanda cha bia cha Serengeti kupitia kinywaji chake cha
Serengeti Premium Lager ambao ndio wafadhili wakuu wa tamasha la Serengeti
Fiesta 2014 wameitaja shoo ya Kigoma kama ya 17 katika ziara zao za mikoani.
Rugambo Meneja chapa wa
kinywaji cha Serengeti Premium Lager aliwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi
na alinaahidi kwamba shoo itakuwa moja
kati ya shoo bora kabisa, aliwataja wanamuziki wa nchini watakaotuimbiza katika
shoo hiyo itakayofanyika katika viwanja vya Lake Tanganyika.
Baadhi ya waliodhibitisha
kufanya shoo hiyo ni pamoja na Ali Kiba, Stamina, Ney wa Mitego, Linah, Recho,
Young Killa, Christian Bella, Mwasiti, Dully Sykes, Mo Music, Baraka Da Prince,
Supa Nyotas:- (G-Luck, K-Style and Edo boy)”.
No comments:
Post a Comment