Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 27 October 2014

WAKAZI WA JIJI LA ARUSHA KUNUFAIKA NA MIRADI YA LAPF


Na Mwandishi Wetu, BrotherDanny Blog
Arusha:
Mfuko wa Pensheni wa LAPF umesema kuwa unatarajia kufanya mabadiliko makubwa sana ya mji wa Arusha hasa kwa kujenga majengo ya kisasa ambayo yatatumiwa na wakazi wa pembezoni mwa jiji la Arusha na hivyop kuweza kupunguza msongamano mkubwa wa watu na magari katikati ya jiji,

Hata hivyo, ujenzi huo ambao utaanza hivi karibuni utaweza kuwa na faida kubwa sana hasa kwa jiji la Arusha kwani nao utachangia kwa kiwango kikubwa ongezeko la pato la taifa.
Hayo yamelezwa na profesa hasa mlawa  ambaye ni mwenyekiti wa bodi ya mfuko huo mapema wakati akiongea na wadau wa mfuko huo katika ufunguzi wa mkutano huo sanjari na maazimisho ya miaka 7o ya mfuko huo.
Profesa hasa  alisema kuwa ujenzi huo wa majengo ya kisasa utaanza rasmi katika maeneo ya Burka kisongo na katika eneo la Usa River ambapo ujenzi huo utaweza kubadilisha historia ya mji wa Arusha.
"Arusha ni mji ambao kwa kweli unakuwa kwa kasi sana na unahitaji uwekezaji wa majengo hasa maduka makubwa kwa hiyo sisi tumeamua kuja kuwekeza katika mji huu ili kuweza kupunguza hata msongamano lakini pia hata kuweza kuwahudumia watu walioko nje ya mji," aliongeza.
Wakati huo huo, alidai kuwa wanawekeza katika mji wa Arusha lakini hata kwenye miji mingine ili kuweza kusaidia Halmashauri kujua namna na mbinu mbalimbali ambazo wanaweza kuzitumia ili kuwekeza hasa kwenye majengo na miradi mikubwa .
"Sisi sio wachoyo hata kidogo kitu ambacho tunakifanya ni kutaka kuona kuwa baada ya sisi kuwekeza tunashirikiana na halmashauri nao wawez kuiga ujuzi na hatua ambazo tumezifanya kusudi nao wakawekeze huko kwao," aliongeza.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), *Hawa Ghasia*,alisema kuwa pamoja na kuwa mfuko huo umeweza kubuni miradi mbalimbali ambayo inawasaidia watanzania lakini bado wanahitajika kuangalia namna ya kusaidia sekta ambazo sio rasmi.

No comments:

Post a Comment