Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday, 30 October 2014

KAMPENI YA TUSKER YAENDELEA KILIMANJARO, MWANZA

Meneja masoko wa Tusker Lager Anitha Msangi akiongea na wasambazaji wa biaza SBL  kwenye uzinduzi wa kampeni ya Tusker Fanya Kweli mjini Moshi.
Meneja biashara ukanda wa ziwa Avinash akiongea na wasambazaji wa bia za SBL katika uzinduzi wa kampeni ya Tusker Fanya kweli mjini Mwanza.
Meneja wa bia ya Tusker Lager Sialouise N Shayo na wasmabazaji wa bia za SBL pichani wakionyesha muonekano mpy wa bia ya Tusker Lager katika uzinduzi wa kampeni ya Tusker Fanya kweli mjini Mwanza.
Meneja usalama na Afya Emmanuel Ntoma akiongea na wasambazaji wa bia za SBL mjini Moshi katika uzinduzi wa kampeni ya Tusker  Fanya Kweli Mjini humo.
Meneja masoko Orest Mbaga akiongea na wasambazaji wa bia za SBL katika uzinduzi wa kampeni ya Tusker Fanya kweli mjini Moshi.
Meneja masoko Orest Mbaga na wasamabzaji wa bia za SBL katika uzinduzi wa kampeni ya Tusker Fanya kweli mjini Moshi.

Baada ya kuzindua kwa mafanikio kampeni ya Tusker “Fanya Kweli” jijini Dar es Salaam hivi karibu, kampuni ya bia ya Serengeti imezindua tena kampeni hiyo katika mikoa ya Mwanza na Kilimanjaro. 
  Fanya Kweli ni kampeni itakayoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha Tusker Lager na itaendeshwa nchi nzima. Lengo la kampeni hii ni kubadilisha fikra za watanzania ili wawe na shauku ya kujituma katika kujitafutia maendeleo yao ili nao waishi maisha bora.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo jijini Mwanza, Meneja Chapa wa Tusker, Sialouise Shayo alisema, “Kampeni hii ya fanya Kweli imelenga kuwawezesha watanzania kupata fikra mpya za kimaendeleo ili kufikia malengo waliyojiwekea,” shayo aliwaambia wakazi wa Mwanza kwamba Fanya Kweli ipo ili kuwawezesha kufikia malengo yao.
Katika hali tofauti kampeni ya Fanya Kweli pia imezinduliwa Moshi ambapo kampuni ya bia ya Serengeti kupitia chapa yake ya Tusker imezindua kampeni kama hiyo kwa wakazi wa Moshi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mjini Moshi Meneja Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti, Anitha Msangi alisema “kampeni ya Fanya Kweli ina maana kuamsha mwamko mpya na kubadili fikra za watanzania na leo tunawaambia wakazi wa Moshi kuwa ndoto yoyote uliyonayo itafanikishwa”.   
 Katika kuhakikisha watanzania wanailewa vizuri kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti, Ephraim Mafuru alisema “Tunatarajia kuwa na programu katika redio zitakazoendeshwa kwa wiki ambapo watu waliofanya kweli katika sekta mbalimbali wataongelea matatizo,vikwazo walivyokumbana navyo katika safari yao ya kufanya kweli, jinsi gani waliweza kuyatatua na ni wadau gani waliwasaidia kuweza kuvishinda vikwazo hivyo. Pamoja na kampeni hiyo, wanywaji wa bia ya Tusker watapata nafasi ya kushuhudia Fanya Kweli katika promosheni zitakazofanyika kwenye baa mbalimbali, vyombo vya habari na “application” itakayowawezesha wanywaji wa Tusker kujumuika kwa pamoja.

No comments:

Post a Comment