Mashine iliyotumika kuhuisha moyo uliokufa na kisha kuupandikiza kwa mgonjwa.
Madaktari wa Australia wamefanikiwa kuwarejeshea uhai wagonjwa watatu baada ya kupandikizwa moyo uliokufa katika operesheni ya kwanza kufanyika duniani.
Madaktari katika hospitali ya St Vincent mjini Sydney walitumia dawa ya kuzuia kuharibika iliyotengenezwa na Taasisi ya Utafiti wa Moyo ya Victor Chang kwa kupandikiza viungo kwa Michelle Gribilas,mwenye umri wa miaka 57 na Jan Damen mwenye umri wa miaka 44, huku mgonjwa wa tatu akiendelea kupona.
Moyo mmoja, ulisimama mapigo kwa dakika 20 kabla ya kuurejesha katika uhai, ukiwa umewekwa katika mashine na kuuchoma dawa ya kuzuia kuharibika.
Jan Damen, mwenye umri wa miaka 44, (akiwa katika picha na mke wake Silvana) alipandikizwa moyo uliokufa na kuupa uhai.
Wagonjwa wawili waliopandikizwa moyo (Michelle Gribilas, kushoto, na Bwana Damen, katikati) wanazungumza na daktari wa upasuaji Kumud Dhital
Moyo unahuishwa baada ya kupoteza uhai na kupandikizwa. Hospitali hiyo inaamini asilimia 30 za watu watarejeshewa uhai kutokana na kugunduliwa kwa dawa hii, ambayo hupunguza kiwango cha uharibifu kwenye moyo na kuwa tayari kupandikizwa.
Kabla ya operesheni hizi, madaktari wa moyo wamekuwa wakitumia moyo kutoka kwa watu waliokufa kwa asilimia 100 ambao katika uhai wao walitaka viungo vyao vitumiwe na watu wengine wenye kuhitaji, lakini sasa upatikanaji wa moyo utaongezeka zaidi.
Dawa hiyo iliyochukua miaka 12 kuitengeneza, pia inasaidia kuimarisha kazi ya moyo ambao unatolewa baada ya kifo (DCD) wakati ukianzishwa kufanya kazi upya.
Bi Gribilas, ambaye amestaafu na kuishi Campsie kusini magharibi mwa Sydney, amesema ni mtu tofauti kwa sasa baada ya kupandikizwa moyo mpya.
CREDIT: BBC/SWAHILI
No comments:
Post a Comment