Misri imetangaza hali ya hatari katika eneo la Sinai kufuatia kuuawa kwa takriban wanajeshi 31 baada ya mashambulizi mawili yaliyofanyika kwenye vizuizi viwili.
Hayo ndiyo mauaji ya wanajeshi wengi zaidi kuwai kutokea nchini Misri kwa miongo kadha ambapo siku tatu za maombolezi zimetangazwa.
Rais wa Misri Abdul Fattah al Sisi aliitisha mkutano wa baraza la usalama wa kitaifa kujadili hali hiyo.
Wanajeshi 28 waliuawa kwenye shambulizi la bomu karibu na mji ulio kaskazini wa Arish huku wengine wakiuawa na watu waliokuwa na silaha kwenye kizuizi kimoja kilicho eneo hilo.
Mashambuli kutoka kwa makundi ya Jihad yanayolenga vituo vya usalama eneo la Sinai yameongezeka tangu jeshi limuondoe madarakani rais Mohamed Mosri mwaka uliopita.
CREDIT: BBC/SWAHILI
No comments:
Post a Comment