Rais wa Mali anasema atafanya awezalo kuepusha taharuki baada ya mtu wa kwanza kuthibitishwa na ugonjwa wa Ebola nchini humo.
Msichana wa miaka miwili aliyeingizwa Mali kutoka Guinea, alikufa kutokana na ugonjwa huo Ijumaa.
Rais Ibrahim Boubacar Keita alisema kisa hicho hakitamfanya afunge mpaka wa Mali na Guinea.
Juhudi zinafanywa kuwatafuta na kuwaweka karantini watu wote waliomkaribia msichana huyo.
Na Shirika la Afya Duniani, WHO, linasema kuwa idadi ya watu waliothibitishwa rasmi kupata Ebola imepindukia 10,000 ingawa inafikiriwa kuwa idadi halisi ni zaidi sana ya hiyo.
Watu kama 5,000 wamekufa kutokana na ugonjwa huo hadi sasa.
CREDIT: BBC/SWAHILI
No comments:
Post a Comment