Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday, 2 October 2014

RADI YAJERUHI WANAFUNZI 17 MWANZA


Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza,Valentino Mlowola

Wanafunzi 17 wa Shule ya Sekondari Kabuholo wilayani Ilemela jijini Mwanza, wamejeruhiwa na radi kufuatia mvua kubwa ilioyonyeshwa jijini humo kwa saa moja.

Tukio hilo lilitokea jana saa 1.45 asubuhi wakati  radi hiyo ilipowapiga wanafunzi wa kidato cha nne 15, mmoja kidato cha tatu na mwingine kidato cha kwanza.



Akizungumza na NIPASHE jana, Mwalimu wa mazingira wa shule hiyo, Humphrey Massawe, alisema tukio hilo lilitokea wakati wanafunzi hao wakiwa darasani huku mvua kubwa ikiendelea kunyesha na radi hiyo kupiga na kuwajeruhi wanafunzi hao.

“Wakati mvua ikiendelea kunyesha walifika baadhi ya wanafunzi ofisini kwa walimu na kusema wenzao wa kidato cha nne wamepigwa na radi…nilipoenda nikawakuta baadhi yao wakiwa wamepoteza fahamu huku Joyce Juma (19), akiwa amelala chini na ameng’ata ulimi na shati lake likiwa limeungua mgongoni,” alisema Massawe.

Muuguzi wa zamu, Aquilina Shai, alisema waliwapokea wanafunzi 17 kutoka sekondari hiyo, Jofrey Dioniz (19), Joyce Juma (19), Flora Magesa (18), Lucy Jonas, John Bwire (17), Yohana Zabron, Mohamed Edwin, Frank Cuthbert na Asimwe Joseph.

Shai aliwataja wengine kuwa ni Aisha Juma, Lucy David, Hawa Musa, Faraja Richad, Anita Robert, Martha Zakaria na Neema Deus.

“Kati yao 14 miwongoni mwao waliruhusiwa baada ya kutibiwa huku watatu Joyce, Neema na Dioniz wakiwa wamelazwa kutokana na hali zao kuwa mbaya,” alisema Shai.

Hata hivyo, Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola, alisema bado hajapata taarifa kuhusiana na tukio hilo.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment