Kaimu
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante
Olegabriel aliyesimama akifungua Mkutano
Baadhi ya wasambazaji wa Filamu nchini (hawapo pichani)kuhusu kuporomoka kwa bei ya
filamu, wa pili kutoka kushoto ni Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini. Bi. Joyce Fissoo.Mkutano huo ulifanyika jana jijini Dar es Salaam.
Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Wednesday 31 December 2014
AZIMIO KUHUSU PALESTINA LAKATALIWA
Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekataa azimio lililoandaliwa na Palestina ambalo limewasilishwa na Jordan linalopendekeza kusitishwa kwa mpango wa Israel wa kuyakalia maeneo ya Palestina kwa miaka miaka mitatu.
MIILI 40 YAOPOLEWA BAHARINI
Kufuatia kupotea kwa ndege ya shirika la ndege la Asia ndege namba QZ8501At ,miili arobaini imeopolewa kutoka baharini katika utafutaji wa mabaki ya ndege hiyo na utafutaji unaendelea.
KIAMA! BARCELONA YAFUNGIWA KUSAJILI HADI 2016
Shirikisho la soka dunia FIFA limeitupilia mbali rufaa iliyokatwa na klabu ya Barcelona kuhusu kuizuia kusajili kwa kukiuka kanuni ya usajili.
UTAFUTAJI WAENDELEA KWA NDEGE ILIYOPOTEA
Ndugu wa abaria waliopotea kwenye ndege ya AirAsia wakilia kwa uchungu
Zoezi la anga na majini la utafutaji wa ndege ya AirAsia aliyoanguka ikiwa na watu 162 baada ya kuwepo kwa dhoruba katika pwani ya eneo la Borneo siku ya Jumapili imeendelea.
MTOTO WA MIAKA MIWILI AUA MAMA YAKE
Maafisa nchini Marekani wanasema kuwa mtoto mmoja mdogo mvulana wa miaka miwili amempiga risasi kimakosa mama yake mzazi na kumuua ndani ya duka moja kubwa la uuzaji bidhaa la Wal-Mart.
BOKO HARAM WANAVAMIA KIJIJI NA KUUA 15
Wapiganaji wanaodhaniwa kuwa ni Boko Haram wamevamia kijiji Kaskazini mashariki mwa Nigeria na kuua watu takriban 15.
Tuesday 30 December 2014
18 WAPATA BEJI ZA UAMUZI FIFA
Waamuzi 18 wa Tanzania wamepata beji za uamuzi za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa mwaka 2015.
AZAM, MTIBWA, SIMBA, YANGA KUCHEZA MAPINDUZI
Timu za Azam, Mtibwa Sugar, Simba na Yanga zitashiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi inayofanyika kisiwani Zanzibar kuanzia Januari 1 hadi 13 mwakani.
WALIOHUSIKA ESCROW WASIFUMBIWE MACHO-ASKOFU
Na Hastin Liumba, Tabora
SERIKALI imeshauriwa kuwa makini na watendaji wake wanaojali kujinufaisha badala ya kutatua kero zinazowakabili wananchi.
Askofu Paul Meivukie wa kanisa la TAG jimbo la Tabora alisema hayo katika mahojiano maalumu na mwandishi wa gazeti hizi yaliyofanyika katika kanisa la Kitete Christian Center mara baada ya kumalizika kwa ibada.
ALAN IVRINE ATIMULIWA WEST BROM
Timu ya West Brom imemfuta kazi kocha wake Alan Ivrine ambaye amekuwa na klabu hiyo kwa miezi saba tangu apate kibarua hicho.
MAREKANI YATUMA MELI YA KIVITA INDONESIA
Wanamaji kutoka Marekani wamesema kuwa wanapeleka moja ya Manowari ya kivita kutafuta ndege ya AirAsia iliyopotea tangu jumapili katika Bahari za Indonesia.
ABIRIA 100 WA AIR TANZANIA WAKWAMA UWANJA WA NDEGE DAR
Zaidi ya abiria 100 wa ndege ya Air Tanzania wamekwama nchini Tanzania, baada ya safari za shirika hilo la ndege kuarishwa.
KILIMANJARO FC YAISHINDILIA POLISI KILIMANJARO 4-1, LIGI YA KILIMANJARO
Na Fadhili Athumani, Moshi
Ofisa Habari Kilimanjaro FC
HATUA ya sita bora, ligi daraja la tatu, Mkoa wa Kilimanjaro imeendelea juzi kwa mchezo mmoja ambapo Kilimanjaro FC imekurupuka kutoka usingizini na kuitandika Polisi Kilimanjaro 4-1.
MBAO FC YAKAMATA USUKANI SDL
Timu ya Mbao FC ya Mwanza imekamata uongozi wa Kundi B la michuano ya Ligi Daraja la Pili (SDL) baada ya jana (Desemba 27 mwaka huu) kuizamisha JKT Rwamkoma ya Mara mabao 2-1.
LIGI KUU YA VODACOM YAINGIA RAUNDI YA 9
Wakati raundi ya nane ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inakamilika leo (Desemba 29 mwaka huu) kwa mechi tatu, ligi hiyo itaingia raundi ya tisa Januari 3 mwakani kwa mechi tano.
DC MOMBA AWATAKA WAFANYABIASHARA TUNDUMA WASIOGOPE MIKOPO
Baadhi ya washiriki katika mafunzo kwa wajasilia mali yaliyotolewa na Benki ya Posta Tanzania (TPB) ikiwa ni jitihada za benki hiyo kutoa elimu ya namna ya kutumia mikopo na kuelezea fursa zilizopo katika Benki hiyo Tunduma.
Saturday 27 December 2014
NHC YAKABILIANA NA TATIZO LA MOYO NCHINI KWA KUSAIDIA MATIBABU YA WATOTO 53 NCHINI INDIA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati wa hafla fupi iliyofanyika jana Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ya kuwaaga jumla ya watoto 55 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo kati ya 104, waliofadhiliwa na Lions Club ya jijini, kwa ajili ya kwenda kutibiwa nchini India. Watoto hao 55 wa awamu ya kwanza waliondoka nchini jana.
KOREA KASKAZINI YAMTUSI OBAMA
Rais Barrack Obama wa Marekani amefananishwa na tumbili wa msitu wa Tropiki
Korea kaskazini imeilaumu Marekani kutokana na mataizo ya mtandao ambayo yameikumba siku chache zilizopita.
Tume ya taifa ya ulinzi nchini Korea Kaskazini inasema kuwa Marekani inavuruga mifumo ya mitandao ya nchi hiyo huku ikimfananisha Rais wa Marekani Barack Obama na tumbili wa misitu ya tropiki mbali na kumshutumu kwa kuhusika katika kuonyeshwa kwa filamu yenye utata inayojulikana kama The Interview.
MKE WA LAURENT GBAGBO ASHTAKIWA IVORY COAST
Bi Simone Gbagbo
Abidjan, Ivory
Coast
Mke wa rais wa zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo, Bi
Simone Gbagbo, amefikishwa mahakamani kutokana na mashtaka ya kuhusika kwenye
ghasia za baada ya uchaguzi ambapo zaidi ya watu 3,000 waliuawa.
WALIMU KENYA KUANZA MGOMO JANUARI 5
Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Kenya (KNUT) Wilson Sossion
Nairobi, Kenya
CHAMA cha
Walimu Kenya (KNUT) kimeitisha mgomo nchi nzima wa walimu kuanzia Januari 5,
kikieleza kwamba mazongumzo yao na Tume ya Utumishi wa Walimu kuhusu maslahi
yao hayakuzaa matunda.
HANDENI VIJANA SACCOS YAIOMBA SERIKALI KUONGEZA FEDHA KATIKA MFUKO WA MAENDELEO YA VIJANA
Viongozi wa Handeni Vijana SACCOS wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kikosi kazi kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo walipowatembelea kufanya tathmini ya Mkopo waliopewa kutoka Mfuko wa maendeleo ya Vijana.
TAMASHA LA WAFALME: DIAMOND, MZEE YUSUF WALIVYOWEKA HISTORIA DAR LIVE
Diamond Platnumz akisema na mashabiki wake waliofurika Dar Live usiku wa kuamkia leo.
Diamond akiwachombeza mashabiki.
Nyomi ya kufa mtu ndani ya Dar Live.
Diamond akiwa kwenye jukwaa la kupanda na kushuka.
Mfalme Mzee Yusuf on da stage.
Mfalme akiwapa 5 mashabiki wake waliofurika Dar Live.
Mzee Yusuf akiwadatisha mashabiki kwa ngoma zake kali.
Mzee Yusuf akicharaza gitaa.
Diamond akicheza sebene ndani ya Dar Live.
Platnumz akizidi kufanya yake stejini.
Diamond akimtambulisha kwa mashabiki mshindi wa zaidi ya milioni 500 za Big Brother Hotshots, Idris Sultan.
Diamond na Idris wakifanya yao stejini.
Idris Sultan akimtambulisha kwa mashabiki wa Dar Live mshikaji wake aliyekuwa naye kwenye mjengo wa BBA, Samantha wa Afrika Kusini.
Diamond akichana mistari ya wimbo wa Muziki Gani na mshikaji aliyepanda stejini kumwakilisha Nay wa Mitego.
Baada ya mshikaji huyo kufanya makamuzi ya hatari, Diamond aliamua kumpatia shilingi 50,000.
Diamond akizidi kuwapa raha mashabiki wake wa Dar Live.
Nyomi ya kutisha ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live.
Diamond akifanya makamuzi na dansa wake.
Dansa wa Diamond akionyesha umahiri wake stejini.
…Sebene time.
Diamond akilitawala jukwaa kwa sarakasi.
NIMEMALIZA: Diamond baada ya kuwakonga nyoyo mashabiki wake waliofurika Dar Live na wao kuridhika aliamua kupozi nao kwa picha hii.
Ijumaa Sexiest Bachelor anayemaliza muda wake, Yusuf Mlela akiwasalimia mashabiki.
Diamond akisalimia na msanii wa filamu, Yusuf Mlela baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa shindano la Ijumaa Sexiest Bachelor. Taji hilo alikuwa nalo Mlela.
Diamond akipokea tuzo ya Ijumaa Sexiest Bachelor kutoka kwa Mkurugenzi wa Kijumosi Traders Ltd, Mohammed Mustapha.
Mhariri wa Gazeti la Ijumaa waandaaji wa shindano hilo, Amran Kaima akimkabidhi Ijumaa Sexiest Bachelor 2014/15, Diamond Platnumz cheti.
Ijumaa Sexiest Bachelor 2014/15, Diamond Platnumz akipozi na tuzo yake pamoja na cheti.
Mzee Yusuf akikandamiza kinanda wakati wa shoo yake Dar Live.
Mzee Yusuf na vijana wake wakifanya yao stejini.
Mzee Yusuf akionyesha ujuzi wa kucharaza gitaa chini kwa chini.
Mashabiki baada ya kupagawa na shoo ya Mzee Yusuf.
MFALME wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ usiku wa Krismasi amewadhihirishia mashabiki wake kuwa ni mfalme baada ya kufanya makamuzi ya hatari katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem, jijini Dar kwenye Tamasha la Wafalmelililodhaminiwa na VODACOM pamoja na COCACOLA.
Staa huyo aligonga ngoma zake zote na kuzikonga vilivyo nyoyo za mashabiki waliofurika katika uwanja huo wa burudani.
Mbali na Diamond, Mfalme wa Taarab nchini, Mzee Yusuf naye alifanya shoo kali na kuwapagawisha mashabiki waliofika kwa wingi kuliko siku zote katika ukumbi huo wa kisasa wa Dar Live.
(PICHA ZOTE NA MUSA MATEJA / GPL)
Subscribe to:
Posts (Atom)