Kutoka kushoto ni Makamu wa Rais anayeshughulikia Sera na Uhusiano wa BG Tanzania, Mr. John Ulanga, Mkurugenzi Mtendaji wa Young Scientist Tanzania (YST) ambaye piandiye muasisi mwenza, Dk. Gosbert Kamugisha na Naibu Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Brian Nolan wakizungumza na wanahabari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Young Scientists
Tanzania (YST) inayo furaha kuwafahamisha wanafunzi, walimu na watu wote kwa
ujumla kuwa onesho lilikuwa likisubiriwa kwa hamu la YST 2015 litafanyika kwa
siku tatu katika ukumbi wa Diamond Jubilee kuanzia tarehe 5 hadi 7 August 2015.
Hili ni onesho na hitimisho la tafiti za sayansi na tekinologia zilifanywa na
wanafunzi wa sekondari kwa takribani mwaka mmoja. Kwa mara nyingine tena,
wadhamini wakuu wa maonesho haya BG Tanzania na Irish Aid wamewezesha mafanikio
haya.
Ni mafankio
makubwa kwa YST kuweza kuifikia mikoa yote kwa kipindi cha miaka mine. Maonesho
ya YST 2015 yajumisha wanafunzi 240 na walimu 120 kutoka mikoa yote ya Tanzania
Bara na Zanzibar. Kwa siku tatu za maonesho, wanafunzi wataonyesha kazi zao za
ugunduzi na utafiti wa kisayansi kama vile kemia, fizikia na hesabu, biologia
na ekologia, teknologia na sayansi ya jamii. Ingawa kazi hizi zinajumuisha
maeneo mapana ya kisayansi, kazi nyingi zimejikita katika kutafuta ufumbuzi kwa
masuala kama afya, kilimo na usalama wa chakula, usalama, mawasiliano na
uchukuzi, nishati na mazingira, elimu, mahusiano na matatizo ya kijamii.
Bado tuna
changamoto katika kuinua kiwango cha sayansi kwa shule za sekondari hasa
ukizingatia uchache wa wanafunzi wanaosoma sayansi na ufaulu usioridhisha.
Ingawa ufaulu umeanza kuimarika kidogo miaka ya karibuni tatizo kubwa limebaki
kuwa ukosefu wa sayansi kwa vitendo na matumizi ya sayansi katika kuboresha
maisha ya watu....sayansi haiwezi kufanywa kwa kutumia chaki na ubao tu. Maonesho
ya YST 2015 yanajaribu kuonyesha kuwa kufanya sayansi ni raha inayotakiwa
kufanyika kwa vitendo kumaliza matatizo mbalimbali na inaweza kufanyika popote
kwa kutumia vifaa vyovyote. Washiriki wa maonesho ya YST 2015 wataonyesha
kupitia kazi zao kuwa kuna namna ya Tanzania kuondokana na umasikini.
Kama njia ya
kuwashukuru vijana wabunifu, zawadi zitatolewa kwa wanafunzi wenye kazi nzuri
za kisayansi. Takribani wanafunzi 60 watazawadiwa zawadi mbalimbali kama pesa
saslimu, medali, vikombe, vifaa vya maabara, na matengenezo ya library na
vitabu. Wanafunzi 6 watazawadiwa udhamini wa kusoma vyuo vikuu kusoma shahada
za sayansi na teknologia na kuendelea kufanya kazi za kisayansi katika maisha
yao. Washindi wa jumla wa maonesho ya YST 2015, pamoja na kupewa pesa na
udhamini wa masoma ya chuo kikuu, pia watashinda zawadi ya kwenda Ireland na
USA mapema 2016 kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa.
YST 2015 ni onesho
la wanafunzi wenye vipaji katika sayansi. Pia ni ushahidi katika kuimalika kwa
ujuzi wa walimu ambao ni walezi wa wanafunzi hao. Haya yote ni matokeo ya
mafunzo kwa walimu ambayo yamekuwa yakitolewa na YST kwa miaka mine iliyopita. Wanafunzi
wapatao 2,000 kutoka sekondari za Dar es Salaam wamealikwa kutembelea maonesho
na kuja kujionea ubunifu wa vijana wenzao. Wananchi wote wanaalikwa kutembelea
maonesho tarehe 6 na 7 August 2015.

No comments:
Post a Comment