Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 27 July 2015

LOWASSA YULEEEE UKAWA, SASA NI VITA DHIDI YA MAGUFULI!



Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa
Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa 
Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) leo umetangaza kumkaribisha waziri mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya kampuni ya ufuaji umeme wa dharura (Richmond), Edward Lowassa, kujiunga nao katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu.

Kukaribishwa kwa Lowassa, ambaye miaka nane iliyopita alitajwa na Chadema kwamba ni fisadi namba saba katika orodha ya mafisadi wanaoitafuna nchi, kunamaanisha kwamba ikiwa ataridhia, basi atagombea urais kupitia umoja huo, hivyo kupambana na mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Joseph Magufuli katika kinyang'anyiro hicho.
Kwa takriban wiki nzima, Ukawa wamekuwa wakiendesha vikao vya kumpata mgombea atakayesimama kwenye nafasi ya urais, huku jina la Lowassa likitajwa tangu Kamati Kuu ya CCM ilipomtema kwenye mchakato Julai 12, mwaka huu mjini Dodoma.
Ukawa walikuwa wamtangaze mgombea urais jana Jumapili mbele ya waandishi wa habari, lakini kwa sababu zisizofahamika, wakauahirisha mkutano huo ambao ulikuwa ufanyike kwenye Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo, leo hii umoja huo umeamua kuuvunja ukimya na kumkaribisha rasmi Laigwanan huku ikitafsiriwa kwamba yeye ndiye atakayepeperusha bendera ya Ukawa kwenye mbio za urais.
Muasisi wa Chadema, Edwin Mtei jana alikaririwa na gazeti la MWANANCHI akimkaribisha mwanasiasa huyo na makada wengine wa CCM kujiunga na chama hicho kikuu cha upinzani.
“Nimesikia Lowassa anatajwa kutaka kujiunga na Chadema, mimi namkaribisha aje, si yeye tu, aje na makada wengine wa CCM kwa kuwa tunapaswa kuimarisha nguvu za kuiondoa CCM madarakani,” alisema.
Akaongeza: “Tunawakaribisha Chadema makada wote wa CCM bila masharti na kama wana nia ya uongozi Chadema ina vikao vya kupitia kulingana na sifa zao na vikao vitakuwa na maamuzi ya mwisho.”

No comments:

Post a Comment