Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 31 July 2015

CHAD 'YAWAUA WAPIGANAJI 100' WA BOKO HARAM


Jeshi la Chad linasema kuwa limewauwa zaidi ya wanamgambo 100 wa Boko Haram katika kipindi cha majuma mawili yaliyopita.

Wanamgambo hao wanasemekana waliuwawa katika makabiliano makali katika visiwa vilivyoko kwenye ziwa Chad.
Aidha taarifa hizo bado hazijathibitishwa.
Kundi la wapiganaji wa Kiislamu wa Boko Haram, lilianzia Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, lakini sasa wanaendesha mapigano katika mataifa kadhaa magharibi mwa Afrika.
Chad imepitisha sheria inayoruhusu kunyongwa kwa watu watakaopatikana na hatia ya kushiriki ugaidi
Alhamisi iliyopita,bunge la Chad lilipitisha sheria iliyoruhusu kunyongwa kwa watu watakaopatikana na hatia ya kushiriki ugaidi.
Hata hivyo wanaharakati wa kupigania haki za kibinadamu nchini humo wanasema kuwa sheria hiyo itatumiwa kuwakandamiza watu.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment