Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 26 July 2015

CHADEMA YATANGAZA MAKADA MAJIMBO MANNE TANGA


NA DEGE MASOLI
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),  kimewatangaza makada watakaopeperusha bendera ya chama hicho katika nafasi ya ubunge wa majimbo manne ya mkoa wa Tanga.
 
Waliopitishwa kupambana na CCM ni David Chanyeghea,  Jimbo la Bumbuli lililokuwa likiongozwa na January Makamba ambaye amechukua fomu  kutetea tena nafasi yake.
 
Chanyeghea amepitishwa jana na mkutano mkuu maalumu wa kura za maoni uliyofanyika mjini Bumbuli baada ya kupata kura 67 na kuwabwaga wenzake watatu waliyokuwa wakiwania nafasi hiyo.
 
Katika jimbo la Mkinga walimpitisha  Recho  Sadick kupeperusha bendera ya Chadema  baada ya kupata kura  103 kati ya  104 zilizopigwa na moja kuharibika.
 
Atakayeipeperusha bendera ya chadema  Jimbo la Korogwe vijijini ni Emanuel  Kimea  baada ya kuwabwaga wapinzani wake wanne wakati Korogwe mji ni Aman  Kimea aliyewashinda wapinzani wake sita.
 
Wakati huo huo, makada 25 wa CCM wamejitokeza  kuomba kuteuliwa kugombea ubunge katika majimbo ya Kilindi na Lushoto.
 
JIMBO LA KILINDI
Makada  15  akiwemo  aliyekuwa mbunge wa jimbo  la Kilindi, Beatrice Shellukindo, wamejitokeza kuwania jimbo hilo.
 
Mwingine ni aliyekuwa mbunge wa kwanza wa jimbo hilo, Juma Kidunda, Aisha Kigoda, Said Mkindawantu, Hemed Magati, Keleni Mngoya, Msilagi  Shaban, Kingazi Kilua na Majiyablulu Grenford.
 
Makada wengine ni Kimweri Mohamed, Rashid Madeni, Athuman Rusewa, Magawa  Ndaro, Juma Mgaza, na Ally  Kidunda.
 
JIMBO LA BUMBULI
Mbunge aliyemaliza muda wake  Jimbo la Bumbuli, January Makamba (CCM) amepata upinzani kutoka kwa makada wawili wa chama hicho, Bakar Mshihili na Abdulkadir Kaniki baada ya kuchukua fomu na kuzirejesha nao wao wakiomba ridhaa ya kuipeperusha bendera katika nafasi ya ubunge.
 
JIMBO  LA LUSHOTO
Henry  Shekifu amepatawapinzani 10 makada waliyojitokeza  kukabiliana na Shekifu ambaye pia ni mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Tanga ni Hamida Kilua, Abdul Mshangama, Riziki Shemdoe, Nyero Hizza, Paulina Jandwa, Prof  Vicent Kihiyo, Evelini Kweka, Emile Sisili na Shaban Bozinia.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment