Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 31 July 2015

LOWASSA KILA KONA, NEC KUANZA KUTOA FOMU ZA URAIS KESHO JUMAMOSI!



Goodluck Eliona na Pamela Chilongola, Mwananchi
Dar es Salaam.
Tume ya Uchaguzi (Nec) imetangaza kuanzia kesho, Jumamosi, wagombea wa nafasi ya urais wataanza kuchukua fomu za kuwania kiti hicho katika zoezi litakalodumu hadi Agosti 21, mwaka huu.
Kwa mujibu wa ratiba ya Nec, vyama vitatu vya United Peoples Democratic Party (UPDP), Tanzania Labour Party (TLP) na Democratic Party (DP) vitafungua pazia kesho.
Akitoa taarifa ya kuanza kwa uchukuaji wa fomu hizo leo, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva alisema kuwa UPDP kitachukua fomu hizo saa tatu asububuhi, kikifuatiwa na TLP saa sita mchana na DP kitafika katika ofisi hizo saa nane mchana.
Lubuva alisema kuwa Agosti 4, mwaka huu Chama Cha Mapinduzi (CCM) watakwenda kuchukua fomu hizo saa saa sita mchana, saa tatu asubuhi, Agosti 5 itakuwa zamu ya Alliance for Democratic Change (ADC), Tanzania Democratic Alliance (TADEA) huku  Alliance for Change and Transparency (ACT- Wazalendo) wakitarajiwa kuchukua fomu hizo Agosti 17 mwaka huu.
“Baadhi ya vyama vya siasa vimesema vinakuja na wanachama wao kuchukua fomu kwa shamrashamra. Shamra shamra ziwepo lakini zisivunje amani ya wananchi, haki hiyo isifanywe kukatiza uhuru wa watu wengine,” alisema Lubuva.
Mwenyekiti huyo ambaye aliambatana na Kamishna wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, amesema kutokana na idadi kubwa ya wanachama wanaoweza kujitokeza wakati wa kuchukua fomu hizo zinazotarajiwa kurejeshwa kabla ya Agosti 21, mwaka huu, wagombea na watu wachache pekee ndio watakao ruhusiwa kuingia ndani kuchukua fomu ili shughuli nyingine katika jengo hilo zisisimame.
Lubuva ameongeza kuwa ni vema wagombea urais wachukue fomu hizo mapema ili waweze kuwatafuta wadhamini wasiopungua 200 katika mikoa minane bara na miwili visiwani.
Pia, Nec imewaonya wanasiasa wanaotoa matamshi yenye uchozezi huku akitolea mfano maneno yaliyotamkwa na kiongozi mmoja wa chama cha siasa kuwa chama chake kitashinda Uchaguzi Mkuu ujao hata kwa goli la mkono.
“Viongozi wawe makini wasitoe matamshi yanayoweza kuleta tafsiri mbaya. Goli la mkono ni matamshi yasiyo na breki,” amesema Jaji Lubuva.
Vile vile, Lubuva amewataka wananchi kutokubali kutoa kadi zao za kupigia kura kwa ajili ya kupewa mikopo, kama ambavyo kundi moja la vijana limedaiwa kufanya katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Mkuu wa Idara ya Uendeshaji Uchaguzi, Clothilde Komba alisema kuwa wagombea wote watachukua fomu hizo bila malipo, lakini watapaswa kutoa Sh1milioni kwa mgombea wa urais, Sh50, 000 kwa kiti cha ubunge na Sh5, 000 kwa udiwani.
Akizungumzia mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu hizo, Kova alisema kuwa wagombea wa vyama vyote wanatakiwa kutumia Barabara ya Obama, kisha watawaacha wapambe wao katika eneo la Gymkhana.
Pia, Kova amesema polisi itaongeza idadi ya askari wakati wagombea watakapokuwa wakichukua na kurudisha fomu katika barabara watakazopita ili shughuli nyingine ziendelee kama kawaida.
“Kama kuna viongozi na wanachama wao watakaoonyesha kukaidi jeshi la polisi halitasita kuchukua hatua za kisheria,” Kova amesisitiza.
CREDIT: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment