Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 30 July 2015

AGATHON RWASA NAIBU WA SPIKA BURUNDI

Agathon Rwasa achaguliwa Naibu Spika
Hii leo bunge lipya lililochaguliwa nchini Burundi limewateua viongozi wake.

Licha ya kupinga uchaguzi mkuu wa hivi majuzi kiongozi wa upinzani Agathon Rwasa amekubali kuwa naibu wa spika.
Wadhifa wa spika umekabidhiwa mwenyekiti wa chama kinachotawala CNDD FDD Pascal Nyabenda.
Rwasa alijipatia kura 108 kati ya 112 baada ya kupata uungwaji mkono na chama cha CNDD-FDD.
Baada ya uteuzi wa leo, imebainika wazi kuwa uongozi wa bunge hilo utatawaliwa na wanaume kutokana na kuondolewa sheria ya ndani walioweka kuwa lazima kuwe na uakilishi wa wanawake japo mmoja, katika uongozi wa bunge hilo.
Rwasa alijipatia kura 108 kati ya 112 baada ya kupata uungwaji mkono na chama cha CNDD-FDD.
Zaidi ya watu 70 walipoteza maisha yao baada ya makabiliano kati ya wafuasi wa rais Pierre Nkurunziza na wapinzani waliomtaka asigombee kiti muhula wa tatu wa urais.
Rais Nkurunziza alishinda kwa asilimia 70 ya kura
Wapinzani walidai kuwa muhula huo unakiuka sheria za nchini.
Naye rais Nkurunziza alishikilia kuwa muhula wa kwanza hakuchaguliwa na watu ,kwa hivyo haikuwa kinyume na sheria kwake kuwania muhula mwengine wa urais.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment