Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 26 July 2015

HAIJAWAHI KUTOKEA, ZIARA YA RAIS OBAMA NCHINI KENYA NI BALAA!

RAIS OBAMA NA MWENZAKE UHURU KENYATTA HATIMAYE WAMEFUNGUA KONGAMANO LA SITA LA KIMATAIFA KUHUSU UJASIRIAMALI KATIKA MAKAO MAKUU YA UMOJA WA MATAIFA MJINI NAIROBI.
17.10pm:-Nchini Burundi nawataka viongozi kuketi chini na kujadiliana ili kupunguza umwagikaji wa damu wa aina yoyote.Kenya vilevile itashirikiana na Marekani katika kukabiliana na magonjwa ili kuzuia milipuko.Serikali haifai kuwatenga watu kulingana na jinsia zao kwa kuwa wao wana haki kama watu wengine.
Obama
17.01pm:-Tishio la Ugaidi-wakenya wameonyesha uvumilivu wa kukabiliana na tatizo hilo.Tunaishukuru Kenya kwa kuwahifadhi wakimbizi wengi wa Somalia.Tumezungumza kuhusu kukabiliana na itikadi kali.Mataifa yetu yatafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa ili kufanikiwa
16.55pm:-Pia tunampango wa kushirikiana na serikali kuleta umeme katika maeneo ya mashamabani.kwa pamoja tunakabiliwa na tishio la maendeleo, nampongeza rais Uhuru kenyatta kukabiliana na Ufisadi.
16.53pm:-Ndege za moja kwa moja kutoka Marekani hadi Kenya-Tunataraji kwamba hili litaangaziwa na safari hizo kuanza hivi karibuni,lakini kuna baadhi ya maswala ambayo ni sharti yaangaziwe ikiwemo mambo ya usalama kabla hilo kutimizwa.Tutaongeza makubaliano yetu ya Agoa kwa miaka mingine kumi ili kuimarisha uhusiano wetu wa kibiashara.
16.50pm:Barrack Obama
Obama
Mazungumnzo yetu yanahusisha maslahi ya mataifa yetu.Mwanzo naipongeza Kenya kwa kuimarisha demokrasia nchini.Uchaguzi uliofanyika ulikuwa wa ushindani mkubwa na wa amani.Nitakutana na wawakilishi wa vyama vya kijamii kwa kuwa wao ni kitengo muhimu katika kupigania demokrasia.Vita dhidi ya wawindaji haramu-tuna mpango wa kuweka sheria inayopiga marufuku uuzaji wa pembe za ndovu.Hali ni mbaya nchini Sudan,tunataka vionbozi wa taifa hilo kuweka taifa mbele.
16.47pm:-Marekani na Kenya zina utamaduni tofauti na kwamba kuna maswala muhimu yanayowaathiri wakenya kama vile afya ya uma njaa na umasikini,maswala ambayo yanapewa kipao mbele.Swala la wapenzi wa jinsia moja sio swala muhimu na haliwezi kupewa kipao mbele.
16.46pm:Uhuru-Hatuungi mkono wapenzi wa Jinsia moja
Uhuru Kenyatta
Tunazungumza kwa sauti moja kuhusu maswala mengi sana.Walio katika nyadhfa serikalini ni lazima wawajibike.Tumekubaliana kushirikiana katika mambo mengi ikiwemo kilimo,miundombinu na kawi kwa lengo la Kuimarisha mazingira yatakayovutia uwekezaji.
16.45pm:Obama na Uhuru wajitokeza kuhutubia vyombo vya habari
16.10pm:Mkutano na wanahabari
Ikulu
Mkutano na vyombo vya habari kufanyika mda wowote kuanzia sasa
15.25pm:-William Ruto anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kivita katika mahakama ya ICC mjini the Hague.
15.30pm:Ruto na Obama
Ruto
Hatimaye naibu wa rais wa Kenya William Ruto amefanikiwa kusalimiana na rais wa Marekani Barrack Obama baada ya kukosekana hapo jana katika ujumbe uliomkaribisha rais huyo alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.
15.15pm:Mkutano na wanahabari
Umati uliomsubiri Obama barabarani
Baada ya kikao hicho cha faragha kati ya serikali ya Kenya na Marekani Viongozi wa mataifa hayo Rais Barrack Obama na Mwenzake wa Kenya watafanya mkutano na wanahabari ili kuweza kutangaza yale walioafikiana katika mkutano huo wa kibiashara
15.00pm:Ikulu ya rais Nairobi kenya
Ikulu
Mkutano wa faragha wa kibiashara kati ya mataifa ya kenya na Marekani umeanza katika ikulu ya rais nchini Kenya.Rais Barrack Obama na mwenzake wa Kenya Uhuru Kenyatta wanawaongoza wajumbe kutoka mataifa hayo mawili katika mkutano huo.Swala la ugaidi ni miongoni mwa maswala tata yanayotarajiwa kujadiliwa katika kikao hicho.
Watu waliovalia nguo zenye rangi za bendera ya Marekani
Rais ‪Obama‬ pia anatarajiwa kutia sahihi ya mikataba ya kibiashara na mwenyeji wake rais Kenyatta katika ikulu ya Nairobi
14.30pm:Ikulu ya rais Nairobi
Ruto
Rais Barrack Obama kukutana na naibu wa rais wa kenya William Ruto ambaye anakabiliwa na mashataka ya uhalifu wa kivita katika mahakama ya kimataifa ya ICC katika mazungumzo ya kibiashara kati ya Kenya na Marekani yatakayoandaliwa katika ikulu ya rais
13.50pm:Rais Obama akiweka maua
Obama
Rais Barrack Obama akiweka shada la maua katika eneo la kumbukumbu ya mauaji ya kigaidi katika uliokuwa ubalozi wa Marekani katikati ya jiji la Nairobi
13.25:Memorial Park
Obama
Obama
Rais Obama na Uhuru Kenyatta wawasili katika eneo la shambulizi la kigaidi katika uliokuwa ubalozi wa Marekani katikati ya jiji la Nairobi.Baadhi ya barabara katika jiji la Nairobi zimebakia kuwa mahame
13.10pm:Manusura 1998
Manusura
manusura
Raia Walionusurika shambulizi la 1998 kenya wabeba mabango wakidai kwamba hawakufidiwa.Wanamtaka rais Obama kutowatupa na badala yake kuangalia maslahi yao.
12.45pm:Densi
Wachezaji densi
Nairobi
Wachezaji densi ya kimasai wakisubiri kumtumbuiza rais Barrack Obama aliyetarajiwa kuwatembelea katikati ya jiji la Nairobi
12.30pm:M-kopa
M-kopa
Rais Obama kwa sasa ametembelea maonyesho ya uvumbuzi jijini Nairobi ambapo alikutana na June Muli afisa anayesimamia maslahi ya wateja M-Kopa ambao hutoa huduma ya kawi ya jua ya 'pay as you go' katika makaazi.
11.10am:Memorial Park
Obama-uhuru
Obama na Uhuru sasa waelekea katika eneo la shambulizi la kigaidi la mwaka 1998 jijini Nairobi
10.55am:
Obama na Uhuru
Obama amaliza hotuba yake
10.50am:BBC hewani moja kwa moja
Obama
Runinga ya BBC inapeperusha moja kwa moja kongamano hilo hewani
10.48am:Mpesa
Obama
Kenya inaongoza katika teknolojia za kibiashara.Kwa mfano utumizi wa Mpesa-ni vyema kwamba teknolojia hiyo ilianza hapa Kenya
Obama akiwasikiza wajasiria mali
Obama 'Tutazindua mfuko wa kudhamini biashara zinazoanzishwa na wanawake
Kina mama ndio injini ya maendeleo barani Afrika.
Vibonzo nchini Kenya
Vituo vitatu vitafunguliwa Mali,Kenya na Zambia barani Afrika ili kuwasaidia wanawake wajasiriamali
10.41am:Rais Obama
Rais Obama
Rais Obama awasalimia wakenya kwa neno 'niaje' na
Hawayuni na kusema kuwa familia yake inatoka nchini kenya.
Lengo la mkutano huu aliouzindua miaka mitano iliopita mjini Washington ni kuwapiga jeki wafanyibiashara duniani.
Amesema kuwa kuna umuhimu wa kukabiliana na ufisadi ili biashara kushamiri.
10.35am:Uhuru Kenyatta
Obama
Kenya ilikumbwa na chanagamoto chungu nzima ikiwemo majanga lakini imesimama imara na kusonga mbele.
Bara la Afrika haliwezi kutegemea mataifa ya magharibi .
Taifa la kenya ni chimbuko la makabila tofauti.
Rais Obama
10.15am:Mkutano waanza
Mkutano wa wajasiriamali umeanza katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini Nairobi huku Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akihutubia mkutano
10.00am:Msafara wa Rais Uhuru Kenyatta
Uhuru Kenyatta
Msafara wa Rais Uhuru Kenyatta ukiwa tayari umewasili katika eneo la mkutano wa wajisiriamali unaotarajiwa kufunguliwa na raia wa marekani Barrack Obama
09.45am:Waandishi
Waandishi habari
Waandishi
Waandishi wa habari wakijiandaa kuliangazia kongamano la kibiashara la wajasiriamali katika eneo la Gigiri jini Nairobi.Vifaa vya waandishi hao vimepekuliwa na maafisa wa usalama wa Marekani.
09.00am:Ndege Nairobi
Ndege za kijeshi
Ndege za kijeshi za Marekani zimeanza kuzunguka katika anga ya jiji la Nairobi kuimarisha usalama.
08.30am:Barabara za Jijini Nairobi:
barabara
Barabara nyingi za mji wa Nairobi zimeonekana kuwa bila watu na magari kufuatia kuwasili kwa rais Obama.Mapema leo maafisa wa polisi walionekana katika barabara zinazoelekea katika eneo la Gigiri ambapo rais Obama atafungua rasmi kongamano la kibiashara.
08.20am:Obama na familia yake
Sara Obama,Barrack Obama na Daktari Auma
Mama Sarah Obama,Rais Obama na dadaake Daktari Auma Obama wakijumuika katika chakula cha jioni katika hoteli moja jijini Nairobi.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment