Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 26 July 2015

MRAMBA, YONA WAKATA RUFAA

Mawaziri waandamizi wa zamani, Basil Mramba (Kushoto) na Daniel Yona (Kulia)

NA ROMANA MALLYA
Mawaziri waandamizi  wa zamani,  Basil Mramba na  Daniel Yona jana wamekata rufaa katika Mahakama Kuu ya Tanzania, kupinga hukumu iliyotolewa dhidi yao ya kwenda jela miaka mitatu na kulipa faini ya Shilingi milioni tano.
 
Hukumu hiyo ilitolewa Julai 6, mwaka huu na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu chini ya jopo la mahakimu watatu ambao ni Hakimu Saul Kinemela, Jaji Sam Rumanyika na Jaji John Utamwa baada ya kukutwa na hatia ya mashtaka mawili ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Sh. bilioni 11.7.
 
Baada ya hukumu hiyo, jana Wakili wa Serikali Timothy Vitalis, alisema mahakamani hapo kuwa, chini ya timu ya mawakili, waliwasilisha maombi ya kukata rufaa wakitaja upungufu wa aina tatu kwenye mwenendo wa kesi iliyopita.
Upungufu huo uliosababisha kukata rufaa ni kutokana na hati ya mashtaka haikuwa sahihi, ilikuwa na kasoro.
 
Alitaja eneo la pili lililosababisha kukata rufaa kuwa ni ushahidi wa Jamhuri haukuwa na uzito wa kuwatia hatiani na mwisho ni adhabu iliyotolewa ilikuwa ni kubwa.
 
Wakili mwingine upande wa utetezi, Cuthbeth Tenga, alisema wateja wao hawakuridhika na mwenendo wa kesi ulivyoendeshwa na majaji ambao ni Rumanyika na Kinemela wa mahakama ya Kisutu.
 
Katika rufaa hiyo, Jaji wa mahakama hiyo, Salvatory Bongole, alipoitaja aliieleza mahakama kuwa, hataweza kuendelea na kesi hiyo kwa sababu mmoja wa waliokata rufaa anafahamiana naye.
 
Aidha, Jaji Bongole aliiambia mahakama kuwa, kesi hiyo itasikilizwa Julai 31, mwaka huu kwa sababu anayetarajia kuiendesha atatoa nje ya mkoa wa Dar es Salaam.
 
Katika hukumu hiyo, mahakama ya Kisutu ikimwachia huru aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Gray Mgonja baada ya kumuona hana hatia.
 
Washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza mwaka 2008 wakikabiliwa na mashitaka ya kuisababishia serikali hasara ya kiasi hicho cha fedha kutokana na kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya kukagua madini ya dhahabu ya M/S Alex Stewart ya Uingereza.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment