Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday, 30 July 2015

KENYA AIRWAYS YATANGAZA HASARA KUBWA


Shirika la ndege la Kenya Airways (KQ) limetangaza hasara kubwa ya Shilingi bilioni 25.7 za Kenya sawa na dola milioni 257 katika kipindi cha fedha cha mwaka wa 2014-2015.

Hii ni hasara ya asilimia 661% ikilinganishwa na kipindi cha fedha cha mwaka wa 2013-2014.
Mwaka uliopita kampuni hiyo ya ndege ilitangaza kuwa imepata hasara kubwa wakati huo ya shilingi bilioni 3.3 mwaka uliopita wa kifedha.
Uongozi wa shirika hilo unasema kuwa hasara hii kubwa imetokana na kuporomoka kwa thamani ya sarafu ya Kenya.
Shilingi ya Kenya imeporomoka kwa asilimia 11 ya thamani yake katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita miongoni mwa sababu zingine.
''Ushindani kutoka kwa mashirika ya ndege kutoka ghuba na mashariki ya kati, mbali na swala kuu la ugaidi imechangia pakubwa hasara kubwa tuliyopata ''alisema Mkurugenzi mkuu mtendaji Mr. Mbuvi Ngunze.
Mkurugenzi mkuu mtendaji Mr. Mbuvi Ngunze amechukua juzi wadhfa huo kutoka kwa Titus Naikuni
Bwana Ngunze ambaye amechukua wadhfa huo mwezi Desemba mwaka uliopita kutoka kwa mkurugenzi mkuu wa kipindi kirefu Dr. Titus Naikuni, anasema kuwa Kenya Airways imekumbwa na msukosuko wa masoko yake kwani yaliathirika na ugonjwa wa Ebola kwa kipindi kirefu cha mwaka uliopita, na mfumuko wa bei ya mafuta katika soko la dunia.
Habari hii sio nzuri kwa wenye hisa wakuu ambao ni Serikali ya Kenya ambayo tayari, ilikuwa imeipa shirika hilo la KQ mkopo zaidi wa shilingi bilioni 4.2 za Kenya ilikuisaidia kurejesha ushindani wake na kuiwezesha kulipa mishahara wafanyikazi wake.
Kulingana na shirika hilo kurejea kwao katika soko lake la Magharibi mwa Afrika kutaiwezesha kuleta faida tena.
KQ vilevile iko mbioni kutafuta mkopo zaidi wa dola milioni 200m kutoka kwa benki ya Afrexim ilikuiwezesha kutekeleza wajibu wake kabla ya kutathmini kima cha madeni yake.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment