Mwenyekiti wa Chama cha Albino nchini (TAS), Ernest Kimaya akimshukuru Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro (katikati meza kuu), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (hayupo pichani), Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu (kulia meza kuu), kwa msaada wao ambao umesaidia matukio ya utekaji na mauaji ya albino kupungua kwa kiasi kikubwa. Pia alisema Kamati iliyozinduliwa itaongeza nguvu zaidi katika kukabiliana na changamoto ambazo zinawakabili za usalama wao nchini. Kushoto meza kuu ni Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi. Kamati hiyo ilizinduliwa na Waziri Dk. Migiro kwa niaba ya Waziri Chikawe, katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro akizungumza na Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi (kulia), na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu mara baada ya kupokelewa Waziri huyo katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ili azindue Kamati itakayoshughulikia changamoto za usalama za watu wenye Ualbino nchini, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Kamati hiyo imeundwa kutokana na ahadi ya Rais Jakaya Kikwete alipoitoa alipokutana na viongozi wa Chama cha Albino nchini (TAS), Machi 5, mwaka huu. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro (wanne kulia-mstari wa mbele), Kaimu
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi (katikati), na Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu (watatu kulia) wakiwa katika picha
ya pamoja na wajumbe wa mkutano wa uzinduzi wa Kamati itakayoshughulikia
changamoto za usalama za watu wenye Ualbino nchini. Kamati hiyo ilizinduliwa na
Waziri Migiro kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Hata
hivyo Kamati hiyo imeundwa kutokana na ahadi ya Rais Jakaya Kikwete alipoitoa
alipokutana na viongozi wa Chama cha Albino nchini (TAS), Machi 5, mwaka huu.
Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Picha
zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment