Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 30 July 2015

TFF YAIPONGEZA AZAM FC

Wachezaji wa Azam FC wakishangilia ushindi wao wa penalti 5-3 dhidi ya Yanga kwenye robo fainali ya Kombe la Kagame jana, Jumatano Julai 29, 2015.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi ametuma salam za pongezi kwa klabu ya Azam FC kwa kufanikiwa kuingia katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Kagame inayotimua vumbi jijini Dar es salam.
 
Katika salamu zake kwa uongozi wa klabu ya Azam, Malinzi amewataka kutobweteka na kuongeza bidii katika hatua hiyo ya nusu fainali ili waweze kufuzu kwa hatua ya fainali na kutwaa Ubingwa huo na kuwaomba watanzania wote kuwasapoti wawakilishi pekee wa nchi kwenye michuano hiyo

TFF kwa niaba ya familia ya mpira na watanzania wote, inatwakia kila la kheri Azam FC katika mchezo wake wa kesho wa nusu fainali dhidi ya KCCA.

No comments:

Post a Comment