Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 25 July 2015

WABUNGE WA ZAMANI WAPETA VITI MAALUM – TABORA.

Munde Tambwe

Na Hastin Liumba, TaboraMBUNGE aliyemaliza muda wake viti maalum kupitia Chama cha Mapinduzi – CCM  Munde  Tambwe  amefakiniwa kutetea kiti chake kwa kupata ushindi baada ya kuwashinda wapinzani wake saba.

Katika mkutano huo maalum wa uchaguzi wa UWT mkoa uliofanyika ukumbi wa chuo cha utumishi wa umma mjini Tabora  Munde alishinda uchaguzi huo kwa kupa jumla ya kura 662.

Nafasi ya pili katika uchaguzi huo imechukuliwa na aliyewahi pia kuwa mbunge wa viti maaluum Mwanne Mchenba aliyepata kura 342 huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Aziza Ally kwa kura 290.

Akizungumzia mkutano huo katibu wa CCM wilaya ya Tabora mjini Kanuti Ndaghine ambaye pia anakaimu nafasi ya katibu wa mkoa  amesema uliendeshwa kwa haki kwani hakukuwa na malalamiko yoyote mara baada ya kutangazwa kwa matokeo.

Katibu huyo amewataka washindi wawili wa juu wasibweteke na ushindi waliopata bali wajitahidi kukipigania chama ili kiweze kupata viti vyote vya ubunge wa majimbo yaliyopo mkoani hapa ndipo wawezekupata uhalali wa kuingia bungeni.

Wagombea wengine na kura zao kwenye mabano ni Paskazia Malunde (52), HamidaThabit (40), Asma Suleiyum (40), Nasalile Mwaipase (16) na Agnes Mgongo (6).

No comments:

Post a Comment