Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday, 26 July 2015

MAWAZIRI, WABUNGE WAKABWA KOO MAJIMBONI

Profesa Muhongo
Mawaziri na wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wamepata upinzani mkali katika majimbo wanayoyashikilia na wanayotarajia kuwania katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.
 
Upinzani huo unatokana na wanachama wengi kujitokeza kupambana na vigogo hao ambao wengi wao wamekaa katika majimbo kwa zaidi ya miaka 10.
 
Majimbo yanayokabiliwa na upinzani mkubwa ni yale ya mikoa ya Kanda ya Ziwa na Tanzania Zanzibar.
 
PROF. MUHONGO
Waziri aliyejiuzulu wa Nishati na Madini kwa kashfa ya Tegeta Escrow, Prof. Sospeter Muhongo, ambaye aliingia bungeni kwa kuteuliwa kupitia CCM, amepata upinzani mkali katika jimbo analowania la Musoma Vijijini kwa kujitokeza wagombea wengine wanane.
 
Prof. Muhongo anang’ang’aniwa kwa karibu na mpinzani wake, Anthony Mtaka, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.
 
NIMROD MKONO 
Mbunge aliyekaa madarakani kwa miaka 20 kupitia CCM, Nimrod Mkono, katika Jimbo la Musoma vijijini, anaendelea kupata upinzani mkali kutoka kwa wagombea wa nafasi hiyo katika jimbo jipya la Butiama.
Wagombea 10 walijitokeza kugombea nafasi hiyo ili kupata mshindi mmoja.
 
Mkono ameonekana kupata upinzani mkali kutoka kwa Christopher Siagi ambaye ni mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) Butiama pamoja na afisa ushirika wilaya ya Chato, Mwita Mirumbe.
 
Hata hivyo, kampeni za wagombea hao zilionekana kuingiliwa na ukabila pamoja na umri, huku zikionekana kumlenga Mkono.
 
SAADA MKUYA
Waziri wa Fedha wa Muungano Saada Salum Mkuya amepata wapinzani saba katika jimbo la Welezo.
Waziri Mkuya anachuana na Abass Hassan Juma, Issa Abeid Mussa, Ramadhan Omar Rashid, Salma Hassan Kambi,Vuai Abdallah Khamis na Zahor Saleh Mohamed.
 
HUSSEIN MWINYI
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Hussein Mwinyi, anakabiliwa na mpinzani mmoja, Jafari Khamis Ramadhan katika Jimbo la Kwahani.
 
Manaibu waziri wa serikali hiyo ya Muungano ambao wako katika upinzani mkubwa ndani ya chama hicho ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Perera Ame Silima, anayekabiliwa na wapinzani watatu katika Jimbo la Chumbuni.
Perera anachuana na Himid Mzee Haji, Shaaban Salum Jabir na Ussi Salum Pondeza.
 
Nae Naibu waziri wa Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Abdallah Juma Mabodi anachuana na wapinzani sita katika jimbo la Malindi baada ya jimbo lake la awali jimbo la Rahaleo kuvunjwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar kutokana na idadi ndogo ya watu.
 
Mabodi anachuana na Said Kheri Ame, Kombo Mshenga Zubeir, Abass Ibrahim Sanya, Nassor Khamis Mohamed na Ame Kheri Ame.
 
Wawakilishi na Wabunge wanaotetea nafasi zao wamepata upinzani mkubwa ndani ya chama hicho huku baadhi yao wakigombea nafasi mbili kwa majimbo tofauti.
 
Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi, UVCCM Taifa, Sadifa Juma Khamis amelazimika kugombea nafasi ya ubunge Jimbo la Donge na nafasi ya uwakilishi jimbo la Jang’ombe.
 
Sadifa ambaye anatetea tena nafasi yake ya ubunge Jimbo la Donge Wilaya ya Kaskazini B Unguja, anagombea pia nafasi ya Uwakilishi Jimbo la Jang’ombe Wilaya Mjini Unguja ambaye amepata upinzani mkubwa kwa  kuwa na wapinzani kumi ndani ya CCM. Wapinzani wake ni Suleiman Othman Nyanga, anayetetea tena nafasi hiyo  kwa muda wa miaka 20 kwa nafasi hiyo, Mwatum Mussa Sultani,Othman Shabani Kibwana, Kanal Said Ali Hamad, Abdallah Maulid Diwani, Mohamed Rajab Soud, Ramadhan Hamza Chande, Shehe Othman Mohmed, Idrissa Hussein Mrisho na Mwarabu Mmadi Mwarabu.
 
Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu na Utawala bora,  Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini ambaye ni mwakilishi wa jimbo la la Dimani, amepata wapinzani watano huku mbunge wa jimbo hilo Abdallah Sheria akiwa na wapinzani saba.
 
Waziri huyo anayetetea nafasi yake kwa muda wa miaka 15 anachuana na Ali Amour Ali, Madai Hamadi Makungu,Adam Kessi Said na Muhammed Muhsin Simba wanaogombea Uwakilishi Jimbo la Dimani.
 
Mbunge wa jimbo hilo Abdallah Sheria anatetea nafasi yake tena kwa muda wa miaka mitano ,anachuana na Juma Ali Juma, Mohammed Mwinyi Kombo, Abdulrahman Hassan Mwinshehe, Abdul aziz Juma Nassor, Mohammed Yussuf Nuh na Hafid Ali Tahir wanaogombea nafasi ya ubunge jimbo hilo.
 
Naibu waziri wa Afya Zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo, ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kiembe samaki amepata wapinzani wawili, Mjaaliwa Abdallah Rashia na Suleiman Haroub Suleiman.
 
Kwa nafasi ya ubunge mbunge wa jimbo hilo Waride Bakari Jabu amepata wapinzani 11 ambao ni  Gharib  Mohammed Addy, Salum Ame Ahmeid, Mwanamvua Mfaume Hassan, Mbwana Bakar Juma, Dogo Iddi Mabrouk, Jamila Flavian Mahemba, Husein Ali Mjema, Mwinyi Suleiman Mohammed, Ibrahim Hassanal Mohammedal, Ahmeid Mohammed Mwinyi, Saleh Khamis Twala.
 
George Marato, Butiama na Rahma Suleiman, Zanzibar
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment