Kikosi cha AFC Leopards kilichotwaa ubingwa mwaka 1984. Picha kwa hisani ya kenyapage.net.
Na Daniel Mbega wa www.brotherdanny.com
Mashindano ya
Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati 1984 yalifanyika mwezi Januari katika
miji ya Nairobi na Mombasa nchini Kenya katika miji ya Nairobi na Mombasa kama
ambavyo mtandao wa www.brotherdanny.com
unavyochambua.
Jumla ya timu 10
zilishiriki mashindano hayo yaliyogawanywa kwenye makundi mawili sawia.
Hata hivyo, AFC
Leopards ya Kenya ilifanikiwa kulitwaa taji hilo moja kwa moja baada ya
kushinda katika miaka mitatu mfululizona safari hii ilitwaa ubingwa miguuni mwa
mahasimu wao Gor Mahia kwa kuwanyuka mabao 2-1 kwenye fainali.
Kwenye kundi la
Mombasa kulikuwa na mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga, Small Simba (Zanzibar),
Nkana Red Devils (Zambia), Bereck Power Pack (Malawi), na AFC Leopards (Kenya).
Katika kundi la Nairobi kulikuwa na KCC (Uganda), El-Hilal-Obeid (Sudan),
National Printing Agency (Somalia), Gor Mahia (Kenya) na Rio Tinto (Zimbabwe).
Mashindano hayo
yalikuwa magumu kwa Yanga, kwani mabingwa hao wa Tanzania Bara walionekana
kuelemewa sana.
Katika mchezo
wake wa ufunguzi Januari 21, Yanga ilicheza na Nkana Red Devils na matokeo
yalikuwa kufungwa magoli 2-1, Januari 23 Yanga ikajitupa uwanjani kumenyana na
Bereck Power Pack na kufungwa bao 1-0, Januari 25 tena Yanga ilipambana na
mabingwa watetezi, AFC Leopards ya Kenya na ikafungwa tena bao 1-0 na katika
mechi yake yamwisho dhidi ya Small Simba baada ya kuongoza kwa mabao 2-0 hadi
dakika ya 65, Yanga ilijikuta ikifungwa mabao mawili ya haraka haraka na hivyo
kufanya matokeo kuwa 2-2. Kwa hali hiyo Yanga ikawa imetolewa bila kunusa nusu
fainali.
Katika mashindano
hayo ya 11, timu mbili za Kenya, AFC Leopards na Gor Mahia zilifanikiwa kucheza
fainali na Leopards ikafanikiwa kulitwaa tena kombe hilo.
Hii ilikuwa ni
mara ya pili kwa timu hizo kupambana katika mchezo wa fainali ya michuano hiyo.
Mara ya kwanza kwa timu hizo kukutana katika fainali ilikuwa mwaka 1980 mjini
Blantyre, Malawi ambapo Gor Mahia ilitwaa ubingwa kwa kushinda mabao 3-2.
Hata hivyo, hii
ilikuwa mara ya tatu kwa timu za nchi moja kukutana katika fainali za michuano
hiyo. Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1975 wakati Simba na Yanga za Tanzania
zilipokutana katika mchezo wa fainali huko Zanzibar na Yanga ikafanikiwa kutwaa
ubingwa huo kwa mara ya kwanza kwa kuifunga Simba magoli 2-0.
Kwa kuchunguza
kwa undani zaidi kumbukumbu za nyuma za mashindano hayo, hii ilikuwa mara ya
tano kwa timu za Kenya kukutana katika michuano hiyo na ilikuwa mara ya nne kwa
Gor Mahia na Leopards kumenyana kuwania ubingwa huu.
Mbali na kukutana
katika fainali, timu hizi mbili za Kenya zenye upinzani wa jadi kama Simba na
Yanga za Tanzania, ziliwahi kukutana tena mara mbili.
Mwaka 1982
zilikutana mjini Nairobi katika mchezo wa nusu fainali ambapo hazikufungana,
lakini Leopards ilipewa ushindi baada ya Gor Mahia kugomea sheria ya penati
tano tano.
Mwaka 1983 huko
Zanzibar zilikutana katika kundi B na Leopards ilishinda mabao 2-1. Pia
zimepata kukutana katika mechi za kundi B huko Lilongwe, Malawi mwaka 1980
kabla ya kukutana katika mchezo wa fainali na Leopards ilishinda 1-0 (Wakati
huo ikiitwa Abaluhya FC).
Mara nyingine
tena Gor Mahia na Luo Union (sasa Re-Union) zilikutana katika mashindano hayo
mwaka 1977 mjini Tanga, ambako Luo Union iliyokuwa ikitetea ubingwa wake,
iliifunga Gor Mahia 4-2 katika mechi ya kundi B.
Mwaka 1984 Leopards
ilikuwa na wachezaji wazuri sana kama golikipa Mahmoud Abbas, Mike Weche,
Patrick Shilasi, John Arieno, Josephat Murila, Issa Suleiman, Dan Musuku, Ben
Musuku, Wilberforce Mulamba, Dakta Joe Masiga, Tonny Lidonde, Mike Amwayi,
Haggai Mirakau, Francis Lubembe na Ineah Isabwa.
Kundi A
Gor Mahia 1-1 Kampala City Council
Printing Club 1-1 Rio Tinto
El Hilal 0-3 Gor Mahia
Kampala CC 1-1 Rio Tinto
Rio Tinto 1-1 El Hilal
Gor Mahia 3-0 Printing Club
Printing Club 2-3 Kampala City Council
Gor Mahia 2-0 Rio Tinto
Printing Club 3-3 El Hilal
El Hilal 1-3 Kampala City Council
1.Gor Mahia 4
3 1 0 9-
1 7
[Kenya]
2.Kampala CC 4
2 2 0 8-
5 6
[Uganda]
3.Rio Tinto 4
0 3 1 3-
5 3
[Zimbabwe]
4.Printing Club 4
0 2 2
6-10 2 [Somalia]
5.El Hilal 4
0 2 2
5-10 2 [Sudan]
Kundi B
Yanga 2-1
Nkana Red Devils
AFC Leopards 1-0 Small Simba
Berec PP 1-0 Yanga
Nkana RD 0-0 AFC Leopards
Small Simba 0-0 Berec Power Pack
Yanga 0-1
AFC Leopards
Berec PP 0-2 Nkana Red Devils
Small Simba 2-2 Yanga
AFC
Leopards 0-1 Berec Power Pack
Nkana RD 1-1 Small Simba
1.AFC Leopards 4
2 1 1 2-
1 5
[Kenya]
2.Berec Power Pk. 4 2
1 1 2- 2
5 [Malawi]
3.Nkana Red Dev. 4
1 2 1 4-
3 4
[Zambia]
4.Yanga 4
1 1 2 4-
5 3
[Tanzania]
5.Small Simba 4
0 3 1 3-
4 3
[Zanzibar]
Nusu fainali
AFC Leopards 1-0 Kampala City Council
Gor Mahia 1-0 Berec Power Pack
Mshindi wa tatu
Kampala CC 1-0 Berec Power Pack
Fainali
AFC Leopards 2-1 Gor Mahia
KUMBUKUMBU
HIZI ZIMEANDALIWA NA MTANDAO WA www.brotherdanny.com.
Ukirejea weka chanzo cha habari tafadhali.


No comments:
Post a Comment