Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday, 18 July 2015

MBU WANAWEZAJE KUTAMBUA MWILI WABINADAMU USIKU?


Utafiti mpya umebaini kwamba mbu hutafuta kitu cha kula kwa kutumia vigezo vitatu, harufu, macho na joto.

Utafiti huo unasema kuwa mbu anaweza kufahamu aliko mwanadamu kupitia hewa ya kaboni ambayo watu hupumua nje.
Inasemekana mbu hunusa hewa hii kiasi cha mita 50.
Wanasayansi wamesema kwamba walimfuatilia mbu mwenye njaa, ndani ya mtaro uliofunikiwa.
Kisha waligundua kwamba mbu hao walianza kunusa nusa hewa ya kaboni, na kutema mapovu yenye matone meusi yaliowekwa na watafiti hao sakafuni.
null
Mbu
Imebainika kwamba wakati mbu yuko mita chache karibu na kile anacholenga, huvutiwa sana na joto.
Hii imebainisha kwamba hata hufuata joto hilo na kisha kumshambulia mwanadamu.
Huenda ukapata Malaria au ukaponea lakini utakua na vipele pale vya mbu anapokuuma.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment