Shirika la Ujasusi la Marekani (FBI) linasema kuwa mwanamme ambaye alishambulia kituo kimoja cha kijeshi katika mji wa Chattanooga siku ya Alhamisi alikuwa na bunduki mbili na pia alikuwa amevaa nguo ambazo zilikuwa zimetengenezwa kubeba risasi.
Muhammad Youssef Abdulazeez aliwaua wanajeshi wanne wanamaji kabla ya kuuawa.
Anaripotiwa kuishi eneo la mashariki ya kati kwa kipindi cha mieze saba. FBI inasema kuwa inalichukulia shambulizi hilo kuwa la kigaidi licha ya kuendelea kuchunguza lengo la mauaji hayo.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment