Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 21 July 2015

ECOBANK TANZANIA YAZINDUA RASMI WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

 Wafanyakazi wa Ecobank Tanzania wakikata keki kwa pamoja na wateja wa benki hiyo Bw. Betwel Usio (Katikati) na Anna Swai (wa kwanza kushoto) kuashiria uzinduzi rasmi wa wiki ya huduma kwa wateja katika hafla iliyofanyika kwenye tawi la benki hiyo la Sokoine jijini Dar es salaam.

 Meneja wa benki tawi la Sokoine Bi. Anna Chimalilio akimlisha keki moja ya wateja wa benki hiyo Bw. Betwel Usio wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika kwenye tawi la benki hiyo la Sokoine jijini Dar es salaam.
Wafanyakazi wa Ecobank Tanzania tawi la Sokoine wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja katika hafla ya uzinduzi uliofanyika kwenye tawi la benki hiyo la Sokoine jijini Dar es salaam.

Ecobank Tanzania imezindua rasmi wiki ya huduma kwa wateja kwa mara ya kwanza nchini ambayo itaadhimishwa mara moja kila mwaka. Kampeni hiyo iliyoanza rasmi siku ya leo ni njia mojawapo ya benki hiyo kutoa shukrani kwa wateja wake pamoja na kudhihirisha uthamini wao kwa wateja hao.  
Kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni “Tunashukuru” imezinduliwa rasmi leo kwenye tawi la Sokoine la benki hiyo lililopo barabara ya Sokoine (jengo la Karimjee Jivanjee) na itatumika kipindi kizima cha siku 4 za kampeni hiyo.
Kiini cha kampeni hiyo ya Ecobank Tanzania sio tu kutoa shukurani kwa wateja wake bali pia kutoa nafasi kwa uongozi wa juu wa Ecobank kuwasiliania, kushirikiana, kupokea mawazo na maoni kutoka kwa wateja kwenye upande wa huduma zao pamoja na kupatia ufumbuzi wa baadhi ya malalamiko wanaliyokuwa nayo. Hii ni mara ya kwanza kwa benki hii kuanzisha mpango huu na inategemea kuwa na kampeni kama hii kila mwaka kuanzia mwaka huu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, mkuu wa Ecobank upande wake mkuu wa Idara ya benki za ndani Ecobank Tanzania, Bi. Joyce Malai alisema “Maamuzi ya kila siku ya Benki hii yanahusiana na wateja wetu, wao ndio rasilimali yetu kubwa na hivyo ni muhimu kuhakikisha wanapata huduma nzuri na kubaki wenye furaha”
Aliongezea kuwa duniani kote, Ecobank inatambulika kwa kutoa huduma bora kwa wateja na hivyo Tanzania haina tofauti katika kufikia viwango hivyo.
Kwa upande wake mkuu wa ushiriki wa wateja Ecobank, Bi. Fatna Tambwe alisema msingi wa wiki ya huduma kwa wateja ni kuelimisha wateja njia mbadala za kupata huduma za kibenki kwa nia ya kuwahamisha wateja kutoka matawi ya benki hadi njia hizo mbadala. Hii itakuwa pia fursa ya kupata maoni ya jinsi gani wateja wangependa kuhudumiwa kwa nia ya sisi kujiboresha na kutoa huduma ambazo wateja wetu wanahitaji na hivyo Bi. Fatna aliwasihi wafanyakazi wa Ecobank walitilie jambo hilo maanani wakati wa kampeni hii.
Bi. Fatna aliwasihi wateja pia kutumia kutumia fursa hiyo ili waweze kujua kwa undani kuhusiana na huduma za kielektroniki za benki hiyo kama;- ATM’s, benki kupitia mtandao, vituo vya mawasiliano an vituo vya mauzo ambavyo vitawezesha wateja kupata fedha kwa urahisi na uharaka, kupata taarifa za akaunti zao na pia kufanya miamala bila kuwa na haja ya kutoka nyumbani wala ofisini.

Wakati kampeni hii ya wiki ya huduma kwa wateja inaendelea, nguvu kubwa pia itaelekezwa kuwafundisha wateja kuhusu huduma mpya ya Ecobank MasterCard, iliyopo mbioni kuzinduliwa kwa wateja wake. Benki pia itachukua fursa hii kuwaelimisha wateja wake juu ya huduma mbalimbali za Benki hiyo ili kuhakikisha kuwa wateja wake wanapata uelewa ili wazitumie ipasavyo huduma hizi.

No comments:

Post a Comment