Lucas Lumambo Selelii akiwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati wa Bunge la Tisa.
Na Hastin Liumba, TaboraMAKADA wawili wa CCM wilaya ya Nzega Lucas Lumambo Selelii na Dkt,Hamisi kigwangalla wameonyesha kukabana koo katika kuwania ubunge jimbo la Nzega vijijinni huku sintofahamu ya nani ataibuka kidedea kuteguwa kitendawli hicho.
Dkt,Hamis Kigwangalla alisema shinikizo la kugombea Nzega Vijijini limetoka kwa wananchi wanaotambua umuhimu wake na hivyo walimuomba kugombea eneo hilo.
Alisema endapo chama hicho kitampatia ridhaa ya kupeperusha bendera na kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo atahakikisha wananchi wanapata maendeleo na kuongeza kuwa wachimbaji wadogo wa dhahabu hatochoka kuwatetea.
Kigwangalla alisema katika kipindi cha miaka mitano wananchi wa jimbo la Nzega amewatumikia na kuwapatia maendeleo katika Nyanja za maji,Afya na Elimu.
Kwaupande wake Lucas selelii aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Nzega kwa kipindi cha miaka 15 alichukua fomu kimya kimya katika ofisi hizo za chama wilaya bila kuzungumza na vyombo vya habari.
Hata hivyo inaelezwa jimbo hilo linatarajia kuwa na upinzani mkali kati ya makada hao wawili licha ya kuwepo kwa kada wengine wawili waliojitosa kuchukua fomu za kuwania kiti hicho katika jimbo hilo Jonh Dotto pamoja na Paul Kabelele.
Katika jimbo la Nzega mjini na Hussein Bashe,Joseph Ngulumwa mchuano utakuwa mkali kati ya wawili hao.
Mchuano mkali mwingine utakuwa kati ya Emmanuel Mwakasaka jimbo la Tabora mjini, huku jimbo la Urambo Mashariki mke wa spika wa zamani Samweli Sitta, Magreth Sitta watachuana vikali na Mtumishi kampuni ya Tigo Ali Maswanya.
No comments:
Post a Comment