Mkurugenzi wa Kanda ya Ziwa kutoka Tigo Bw. Ally Maswanya akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kufafanua huduma mbalimbali za TIGO.
Na Hastin Liumba,TaboraJAMII imeaswa kuwalea na kuwatunza watoto yatima ambao muda wote wamekuwa ni wahitaji wa misaada ili waweze kujimu kimaisha.
Hayo yamesemwa na meneja wa Kanda wa kampuni ya simu za mkononi Tigo Ali Maswanya wakati wa chakula maalunmu cha usiku kilichoandaliwa na kampuni ya Tigo mkoani Tabora.
Akizungumza na baadhi ya wageni na watoto yatima wa kituo cha Igambilo Center alisema jamii imewasahau watoto yatima na kujikuta watoto hao wakiishi maisha ya kuomba omba.
Alisema kuwa watoto yatima wana haki kama watoto wengi hivyo wanapaswa kufarijiwa kwa nyakati mbalimbali ikiwa na kushirikishwa katika shuguli za maendeleo.
Kwa upande wake kaimu Mkuu wa Mkoa Suleiman Kumchaya ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Tabora Mjini alisema makampuni mengine yana paswa kujali makundi maalum kwa nyakati mbalimbali nasi katika vipindi vya kama hivyo.
Kumchaya aliitaka jamii kuilinda amani katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu mwezi Octobar mwaka huu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya Tigo kanda ya ziwa Ally Maswanya alisema kampuni hiyo imeamua kushirikiana na waislam pamoja na watoto yatima katika Futari ilikudumisha upendo na waumini wa Dini hiyo.
Alisema kuwa kampuni hiyo imetoa zawadi ya sikukuu ya Iddi kwa watoto yatima iliwaweze kufurahia sikuu hiyo kama watoto wengine waishio na wazazi wao.
No comments:
Post a Comment