Hivi karibuni kampuni ya bia ya
Serengeti imekuwa mstari wa mbele kuleta vipaji vya waimbaji mbalimbali kupitia
tamasha lake la kila mwaka la Serengeti Fiesta.
SBL imeweza kugundua vipaji
mbalimbali kupitia mashindano iliyokuwa ikiyafanya wakati wa matasha hayo kama
vile bonanza la mpira wa miguu na la uimbaji maarufu kama Supa Nyota Divas.
Young Killa ambaye ni moja ya vipaji
vilivyogunduliwa wakati wa matamasha hayo anatarajiwa kuja kuwa mmoja wa mastaa
nyota wa muziki wa hip hop kwani tayari ameshakonga vilivyo nyoyo za mashabiki
katika sehemu mbalimbali ambazo shoo za Serengeti Fiesta zilipita.
Kijana huyo aling’amuliwa katika
tamasha la Serengeti Fiesta lililofanyika Mwanza.
Wakati ziara ya tamasha la Serengeti
Fiesta ikikaribia ukingoni, kulikuwa na maswali mengi toka kwa watu mbalimbali
waliovutiwa kutaka kujua haswa nini maana ya Serengeti Super Nyota Divas na
lengo la mashandino hayo ni nini haswa.
Super Nyota Divas ni shindano ambalo
lilitoa nafasi kwa idadi kubwa ya wasichana kulitumia kuonyesha vipaji vyao katika
kuimba, na kupitia shindano hilo vipaji mbalimbali viling’amuliwa na majaji na
washindi kupatikana.
Kupitia mikoa yote ambayo Serengeti
Fiesta ilipita mwaka huu, kulikuwa na shindano la Super Nyota Divas na hadi
kufikia sasa karibia washindi 15 wamepatikana ambao watasafiri kwenda Dar es
Salaam kushudia shoo ya mwisho ya tamasha hilo.
Kama
sehemu ya washuhudiaji wa shoo, washindi wa Super Nyota Divas hao wapatao 18 wanatarajiwa
kushindana na washindi wengine wa Super Nyota Divas wa mwaka jana jijini Dar es
salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari, mmoja wa washindi wa Super Nyota Divas katika tamasha
la mwaka huu la Serengeti Fiesta hakuficha kuonyesha furaha yake na alikuwa na
kitu cha kusema.
Attu Charles ambaye ni
mshindi wa Super Nyota Diva toka mkoa wa Iringa alisema....”Serengeti Fiesta
2014 imenisaidia kufahamika kama msanii nashukuru kwamba baadhi ya nyimbo zangu
sasa zinapigwa katika vituo mbalimbali vya redio.
Attu pia hakuficha
ukweli kwamba baada ya kuibuka mshindi toka mkoa wa Iringa, wazazi wake sasa
wameamini kwamba ana kipaji cha muziki na kuanza kumsaidia tofauti na
ilivyokuwa hapo mwanzo.
Anna Hillu a.k.a Ania
toka Mwanza alisema.....”Serengeti Fiesta 2014 imenisaidia kujiamini na imenipa
matumaini ya kufanikiwa katika safari yangu ya kimuziki.” Akizungumzia kuhusu
fainali ya shindano la mwisho litakalofanyika Dar es Salaam, Ania
aliendelea....”naamini kuwa kila mmoja ni mshindi kwani matokeo ya kila
msichana alishinda toka katika mkoa wake yalionyesha jinsi yalivyo bora.”
Victoria Sostennes kutoka Moro alisema…”Ninashukuru
kampuni ya bia ya Serengeti kwa kuanzisha aina hii ya mashindano kwasababu
kupitia haya mashindano ndipo kipaji changu kiligunduliwa na sasa siwezi
kusubiri tena kushinda katika fainali itakayofanyika Dar Es Salaam sababu
naamini nina kipaji.
No comments:
Post a Comment