Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday, 1 October 2014

PROF. MUHONGO ASAINI MKATABA WA MRADI WA KUUZIANA UMEME KATI YA ZAMBIA, TANZANIA NA KENYA

Profesa Sospeter Muhongo

Na Anitha Jonas, Maelezo-DSM
WAZIRI wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter Muhongo juzi ametia saini Mkataba wa Mradi kujenga Miundombinu ya kuuziana umeme kati ya Zambia, Tanzania na Kenya (ZTK) katika Mkutano  wa Kumi wa kujadili mradi huo.

Katika utiaji saini Mkataba huo, Profesa Muhongo alisema kuwa mchakato wa kuandaa Mkataba wa mradi huo ulikwishafanyika tangu mwaka 2001 ambapo ulikuwa na vipengele ambavyo kwasasa Mawaziri wa Nishati toka nchi zote tatu wameupitia na umefanyiwa marekebisho. 

Profesa Muhonga alisema kuwa katika marekebisho hayo wamebadili kipengele kilichokuwa kinaeleza juu ya uwepo wa Ofisi moja itakayosimamia mradi huo katika nchi zote tatu, na badala yake wamekubaliana kuwa kila nchi ijisimamie yenyewe badala ya kuwa na Ofisi moja pekee itakayosimamia mradi huo.

“Kwa upande wa Tanzania ujenzi wa mradi huu umeshaanza kazi na mpaka hivi sasa asilimia 90 ya vifaa vya ujenzi wa mradi vimeshawasili katika eneo la ujenzi,” alisema Profesa Muhongo.

Akizungumzia maeneo ambayo mradi huo utapita kwa upande wa Tanzania, Profesa Muhongo alisema kuwa, mradi huo utapita maeneo ya mikoa ya Singida- Arusha-Namanga, na Namanga-Isinya kwa Kenya, kwa upande wa Zambia utapita Mbeya–Iringa na Iringa-Singida-Shinyanga. Ambapo unatarajia kusambaza umeme wa kuanzia 400kV.

Naye Katibu Mkuu wa Nishati nchini Kenya, Mhandisi Joseph Njoroge  alisema kuwa muungano huo wan chi tatu utasaidia kupunguza tatizo la umeme katika nchi zote na Afrika kwa ujumla kwani utapunguza gharama ya umeme pamoja na kuongeza ukuaji wa uchumi katika uzalishaji.

Aidha aliongeza kuwa Serikali yake itahakikisha kuwa Mkataba huo ndani ya siku Thelathini zijazo kabla ya mkutano ujao kuanza, Mwanasheria Mkuu wa Kenya atakuwa umekwisha usaini.

Kwa upande wake Waziri wa Nishati na Madini nchini Zambia, Mh. Christopher Yaruma alisema kuwa nchi yake imeshasaini Mkataba wa kuonyesha dhamira ya kuuziana umeme na nchi ya Malawi, Namibia na Botswana.

Utiaji saini wa Mkataba huo ulihusisha wadau mbalimbali wa maendeleo na wafadhili ikiwemo JICA, COMESA, EU, Korea, Benki ya Dunia, AFD, Ufaransa na Mabalozi wa nchi mbalimbali, ambapo wadau hao wameonyesha nia ya dhati katika kuendelea kuisaidia Serikali hususani katika sekta ya Nishati.

Sambamba na hilo, mkutano wa mwendelezo wa mradi huo badaa ya kuwa umesainiwa na viongozi wa Sheria katika nchi husika unatarajiwa tena kufanyika mwanzoni mwa mwezi wa Kumi na moja nchini Lusaka, Zambia.

No comments:

Post a Comment