NA SALOME KITOMARY
Wabunge 42 wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni (Ukawa), wamepewa adhabu ya kutoingia vikao vyote vya bunge hadi litakapovunjwa na Rais, Julai 9, kulipwa nusu mishahara na posho.
Jumla ya wabunge wa upinzani 90, waliotolewa siku ya kwanza (juzi) ni 11, na jana 35 hivyo kufanya idadi ya waliofukuzwa kuwa 46, huku 43 ambao hawakuwepo ndani ya Bunge kutoguswa na adhabu hiyo.
Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed, alibaki ndani ya Bunge.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya wabunge hao kuwa kwenye harakati za kupinga miswada mitatu ya mafuta na gesi, kuingizwa bungeni kwa hati ya dharura na kujadiliwa kwa pamoja.
Juzi wabunge 11 walitajwa kwa utovu wa nidhamu Bungeni, na kati yao, Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini na Mbunge wa Gando, Khalifa Suleiman Khalifa, wamepewa onyo baada ya kujutia makosa yao.
Waliotimuliwa juzi ni John Mnyika (Ubungo), Tundu Lissu (Singida Mashariki) na Pauline Gekulu ( Viti Maalum) wote wa Chadema.
Wengine ni Filex Mkosamali (Muhambwe) na Moses Machali (Kasulu Mjini) wa NCCR-Mageuzi.
Hadi sasa wabunge 42 wamefukuzwa, huku wawili wakipewa adhabu ya kutohudhuria vikao viwili.
Wabunge hao ni wa Iringa Mjini, Peter Msigwa na Mbunge wa Ole, Rajabu Mbarouk, ambao kesho wataruhusiwa kuhudhuria Bunge.
Miswada iliyozua mtafaruku ni ule wa Sheria ya Petroli wa mwaka 2015, Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesi wa mwaka 2015 na Muswada wa Sheria ya Uwazi na Uwajibikaji katika tasnia ya uchimbaji wa mwaka 2015.
Mbunge wa kwanza kufukuzwa na askari wa Bunge jana ni wa Nyamagana (Chadema), Ezekia Wenje, ambaye mara baada ya Spika kumwita Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, kuendelea na hoja, alitaka mwongozo wa Spika kwamba Azimio la Bunge la Julai 3, mwaka huu, la kuwasimamisha kabisa wabunge watano, siku mbili
(wawili) na watatu kuhojiwa na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, lakini Mbunge wa Mbozi Magharibi, David Silinde, ambaye licha ha Azimio kutomtaja lakini askari walimzuia kuingia katika viwanja vya Bunge.
"Katika maelezo yote ya mwenyekiti wa kamati ya maadili, hakutajwa na katika azimio pia, lakini askari wako wamepewa jina asiingie, tunaposema tunaonewa mnasema tunafanya fujo...ukisoma kanuni ya 86 (7,8), hoja ya Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, unapoleta miswada yote kusomwa kwa wakati mmoja na kujadili ni ukiukwaji wa kanuni," alisema.
Spika Anne Makinda akifafanua hoja hiyo, alisema wabunge hao hawajui kanuni, "nilitamani mjue kusoma kanuni, nilifikiri mnajua kumbe tunamaliza kipindi wala hamjui, mngekuwa mnajua utaratibu wa kupinga kikanuni upo, tumefanya miswada mingi sana inasomwa kwa wakati mmoja...nipeni muda niwaletee orodha ya miswada hiyo."
Alisema kanuni zinaruhusu kwa kuwa maudhui ya miswada ni mmoja, hivyo hakuna kanuni iliyovunjwa.
MAJIBIZANO
Khatib Said Haji: La Silinde hujatoa maamuzi kwanini kazuiwa?
Spika: Wewe ni Silinde, ni kweli kwamba azimio liliruka jina lake, lakini mimi nilimtaja, amehojiwa na kamati na kilichotokea ni makosa ya uchapaji.
Wenje: Mh. Spika lakini wewe hutoi adhabu, azimio la bunge ndilo linatoa, azimio la bunge halikumpa adhabu.
Spika: Wenje mimi sipendi kuchukua hatua zaidi, hizi ni mbinu za kuchelewesha.
Wenje: Hapa tunatafuta haki, na siyo kuchelewesha.
Spika: Kama siyo kuchelewesha basi tokeni nje.
Wenje: Haitakuwa mara ya kwanza mimi kuondolewa ndani ya Bunge hili, nimeshaondolewa mara nyingi.
Spika: Hatuwezi kuendelea huyu anasema na wewe unasema hizo ni adabu?
Wenje: Sisi hatufanyi fujo, wewe ndiyo unatuonea.
Spika: Wewe una adabu gani kusimama mimi nikiwa nimesimama?
Wenje: Nimekaa Mh Spika.
Spika: Sijakupa ruhusa unaongea, itabidi tukutoe nje.
Mabishano yaliendelea kwa dakina tano huku wabunge wa upinzani na Spika wakiwa wamesimama na wabunge hao wakiongea na hivyo Bunge kugeuka kama sokoni huku upande wa upinzani ukidai kuonewa.
Aidha, Spika aliruhusu mwongozo kwa Mbunge wa Mtambile (CUF), Masoud Abdallah Salim, akisema miswada hiyo inahusu suala la Muungano ambao haujashirikishwa na wamewasiliana na Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar ambaye amesema hajui lolote.
Baada ya kauli hiyo, Spika alisema Mbunge huyo ameanza kuchangia muswada na kwa mujibu wa kanuni anaharakisha shughuli.
Mbunge wa Chakechake (CUF), Kombo Khamis Kombo, alisema Bunge ni la wananchi hivyo lazima waliomo wapewe heshima, na kwamba kushindana kwa itikadi za vyama hazitakiwi kuwepo kwani atafukuza wote na siku Rais anavunja Bunge kutakuwa na upande mmoja.
"Naomba mwongozo wako, umekuja katika vita mheshimiwa Spika au umekuja kutuongoza kwa mujibu wa kanuni zetu," alihoji.
Spika: Mh nilidhani una heshima niliyokuwa nakujengea, kumbe huna, nimewaelekeza namna ya kuondoa miswada kwa mujibu wa sheria, nilifikiri unaongoza kumbe unapotosha.
Spika: Kwa mujibu wa kanuni ya 72, Wenje atoke nje, nimeamuru atoke nje na asihudhurie vikao vitano vya Bunge hili.
Aidha, baada ya Wenje kutolewa nje na Askari wa Bunge, wabunge wa upinzani wengine waliendelea kuomba mwongozo huku wakisema "tutoeni wote", na Spika aliwaambia watoke wenyewe lakini walikataa kutoka.
Spika alimuita mtoa hoja, lakini alishindwa kuendelea kutokana na wabunge wa upinzani kugoma kukaa chini.
Baada ya hali hiyo, Spika alisema kwa mujibu wa kanuni ya 74 (1), watapelekwa kwenye kamati ya haki, maadili na madaraka na kutaja majina ya wabunge 18.
Hata hivyo, alitangaza kuahirisha Bunge, huku akiagiza waliotajwa majina kutoka lakini wabunge hao walibaki wamesimama.
Spika alitaja majina mengine ya wabunge tisa, huku Mbunge wa Lindi Mjini, Salum Barwany, akinyoosha mkono akitaka naye atolewe na kubaki wabunge sita, ambao aliwataja kwa pamoja.
Spika alisisitiza kuwa wanatakiwa kutoka na watakuwa nje ya Bunge kwa vikao vitano kwa masharti yale yale ikiwamo kulipwa mshahara na posho nusu.
Aidha, aliwataja wabunge watatu ambao walitoka nje na Bunge kuendelea kwa mawaziri kuwasilisha miswada mitatu.
Bunge hilo linaundwa na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi 261, Chadema 48, CUF 35, NCCR-Mageuzi watano, TLP mmoja na UDP mmoja.
KAULI YA SPIKA KABLA YA KUTOKEA VURUGU
Spika Makinda alisema uamuzi wa kuipanga miswada hiyo kwa pamoja Julai 02, mwaka huu, ulifikiwa na Kamati ya Uongozi katika Kikao chake cha Juni 29, mwaka huu.
Alisema katika vikao vya Kamati ya Uongozi vilivyotangulia, wajumbe wote wa kamati waliohudhuria waliridhika na maelezo ya serikali juu ya umuhimu wa kuleta miswada hiyo kwa hati ya dharura.
"Vilevile Juni 26, mwaka huu, kwa mujibu wa Kanuni ya 85 (1) nilipokea taarifa kutoka kwa Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini Mhe. Murtaza Mangungu, alinitaarifu kuwa kamati imemaliza kazi ya kuchambua na kuijadili miswada husika," alifafanua.
"Kamati iko tayari kuwasilisha bungeni maoni na ushauri wake. Ni baada ya taarifa hii ya Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini ndipo niliagiza miswada hiyo iwekwe kwenye orodha ya shughuli kama kanuni ya 85(2) inavyoelekeza."
Spika Makinda alisema kama wabunge hao walikuwa hawataki miswada hiyo iwasilishwe walitakiwa kuhakikisha kuwa Kamati iliyopewa jukumu la kuchambua Miswada hiyo inaikataa baada ya kujadiliana na serikali kama ilivyokuwa kwenye Muswada wa Haki ya Kupata Habari.
Alisema baada ya mjadala kuanza Bungeni wangeweza kutoa hoja kuwa mjadala usiendelee hadi siku nyingine, ili Mbunge yeyote anayekusudia kuleta marekebisho apate nafasi ya kufanya hivyo.
Alisem kwa kwa kutumia Kanuni ya 90, Waziri mwenye Muswada anaweza akauondoa wakati wowote kabla ya Bunge kuhojiwa kutoa uamuzi na Bunge linaweza kutokuupitisha Muswada husika.
MUSWADA KULETWA KWA HATI YA DHARURA
Spika alisema Miswada kuletwa kwa Hati ya Dharura ni utaratibu wa kawaida na kwamba hatua nyingine zote hufuatwa isipokuwa katika Mkutano huo huo Muswada husoma Mara ya Kwanza na hatua zake zote.
CHANZO CHA TATIZO
Katika semina iliyofanyika Juni 30, mwaka huu, wabunge kwa kauli moja waliungana kupinga miswada hiyo, wakitaka iachwe ijadiliwe na kupitishwa katika Bunge la 11, kwa kuwa muda ni mdogo na wabunge wengi hawana muda wa kuisoma na kujadili.
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Richard Ndassa, alisema atapeleka maoni ya wabunge kwa Spika.
BUNGE KUENDELEA JUMAPILI NA SIKUKUU
Mwanasheria Mkuu wa serikali, George Masaju, aliwasilisha pendekezo la serikali la Bunge kuendelea leo kuanzia saa 5 asubuhi hadi saa 9 mchana, na siku ya sabasaba kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
No comments:
Post a Comment