Mbunge wa Ilemela, Highness Kiwia (kushoto) na Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje wakiwapungia mikono wafuasi wa Chadema walipokuwa wakitoka kuwapokea viongozi wa chama hicho jijini Mwanza jana. Picha na Michael Jamson.
Na Waandishi Wetu
Dar/Mikoani. Baadhi ya wabunge wa Chadema wanaotetea viti vyao wameibuka kidedea katika kura za maoni zilizofanyika katika majimbo mbalimbali nchini jana.
Hao ni pamoja na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ aliyejizolea ushindi mnono wa kura 356 akiwaacha kwa mbali wapinzani wake, Joyce Mashine aliyepata kura43 na Tito Mwanjale kura 18. Wengine waliokuwa wakiwania kuteuliwa na chama hicho ni Lazaro Mwankemwa aliyepata kura 15, Christopher Nyenyembe (12) na Sishe Simbeye (6).
Mbunge mwingine, aliyepata ushindi wa kishindo ni Highness Kiwia wa Ilemela aliyejizolea kura 134 na aliyemfuatia alikuwa Gasper Mwanaliela ambaye alipata kura 28.
Wabunge wengine, Joshua Nassari hakuwa na mpinzani katika Jimbo la Arumeru Mashariki kama ilivyokuwa kwa David Silinde katika Jimbo la Momba.
Tafrani Mbeya Mjini, Mbarali
Awali, kulizuka tafrani iliyotokana na mgombea, Meshack Kapange kuenguliwa. Mgombea huyo alipinga akidai kuwa hakutendewa haki na kwamba kilichofanyika ni kumkingia kifua Sugu.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Chadema Mbeya Mjini, John Mwambigita alisema Kapange alikwishavuliwa uanachama na suala la kuchukua fomu za kuomba ubunge ilikuwa ni haki ya kila mmoja.
Kapange alisema atakata rufaa kwa kuwa hakutendewa haki na wasimamizi wa mchakato huo... “Nimempigia Katibu Mkuu wa Chadema (Dk Willibrod Slaa), akaniambia yuko kwenye mkutano Mwanza, nitampigia kesho (leo) kumweleza kunyang’anywa haki yangu,” alisema. Mzozo mwingine uliibuka Mjini Mbarali baada ya Jidawaya Kazamoyo aliyepata kura 109 kulalamika kuwa ndiye mshindi na kuzuka vurugu zilizosababisha Liberatus Mwang’ombe aliyeshinda kwa tofauti ya kura moja kutolewa nje ya ukumbi akiwa chini ya ulinzi mkali.
Matokeo ya kura ya maoni Chadema
Segerea: Anatropia Theonest (49), Kisheli Mchele 26 Masato Wasira (24), Baraka Sawema (15), Habron Mwakagenda (6), Bakari Yusuph (2), Loyce Gibona (2), Amos Maziku (0), Dominic Orembe (0), George Martin (0).
Lupa: Miraji Hussein amepata kura (65) na kuwashinda wenzake Njelu Kasaka (45) na Fillipo Mwakibinga (32).
Korogwe Mjini: Amani Kimea amewashinda kwa mbali wenzake watano kwa kupata kura 56. Aliyefuata ni Mwakolo Wynjones (26), Calistus Shekibaha (8), Steven Kimea (4), Benson Mramba (1) na Grayson Kibwana (0).
Busega: David Nicad (116), Buluba Mabelele (67), Revocatus Madundo (55), Modest Masunga (4), Sajda Dotto (3), Mapambano Ochalo (2), Keneddy Lufulondama (1), Adam Komanya (0), Lutandula Mabimbi (0) na Mhere Mwita (0).
Sikonge: Godfrey Ndaki (16), Moses Kaombwe (17), Dk Mmeta Yongolo (19), Mtemi Zombwe (70) na Hija Ramadhani 83.
Manyoni: Alute Emmanuel (171) na Thedey Meremeta (47)
Vwawa: Fanuel Mkisi (136), Stephen Mwamengo (42), Solomon Kibona (22), Andrea Bukuku (9), Fadhil Shombe (8), Bob Mwampashe (5) na Jonathan Mwashilindi (5).
Ilemela: Highness Kiwia (134), Gasper Mwanaliela (28), Bugumba Nsumba (20), Wema Dilala (17), Deus Ng’hanyanga (15), Edwin Sarungi (13), Telexphone Masalu (8), Kageshiza Mwendesha (7), Mayalo Kasili (3), Thobias Mogole (7), Magesa Masinde (6), Damas Kimenyi (5), Habath Matalu (5), Greyson Wanzagi (13), Darius Ngocho (5), Humphrey Mmanda (3), Malehe Sweta (3) na Frederick Mataja (2).
Mbozi: Paschal Haonga (82), Fredy Haonga (34), Sophia Mwabenga (18), Ambukusye Kabango (4), Eliud Kibona (3), Anastazia Nzowa (2), Eliud Msongole (1), Seule Nzowa (1) na Zabron Nzunda (1).
Ileje: Emmanuel Mbuba (98), Gwamaka Mbughi (66) na Emmanuel Msyani (37).
Tunduma: Frank Mwajoka (130), Victor Nkonjela (20) na Clemence Nyondo (15).
Momba: David Silinde hakuwa na mpinzani.
Babati Vijijini: Daniel Karenga (14), Esther Sarwatt (17), Herman Sanka (5), Leonard Mao (3), Salum Shawishi (8) na Lawrence Tara (288).
Arumeru Mashariki: Joshua Nassari amepita bila kupingwa.
Makambako: Olaph Mhema (72), Fred Kalonga (57) na Kheri Kisingile (0).
Kibaha Mjini: Michael Mtali (62), Henry Msokwa (38), Ishaka Mnembwe (31), Joachim Mahega (13), Bosco Mfundo (4) na Frank Mzoho (3).
Mbeya Mjini: Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (356) Christopher Nyenyembe (12), Joyce Mashine (43), Lazaro Mwankemwa 15, Tito Mwanjale (18) na Sishe Simbeye (6).
Mbarali: Liberatus Mwang’ombe (110), Jidawaya Kazamoyo (109), Tazan Ndingo (25), Grace Mboka (14) na Dickson Baragasi (9).
Imeandikwa na Raymond Kaminyoge, Julieth Ngarabali, Shaaban Lupimo, Faustine Fabian, Stephano Simbeye na Godfrey Kahango na Brand Nelson.
CREDIT: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment