Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday, 11 July 2015

MEMBE APONGEZWA KUINGIA TANO BORA


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana akizungumza wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) katika ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma jana. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete na Makamu Mwenyekiti Visiwani na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.

Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) katika ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma jana. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Visiwani na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

SIASA SIO UADUI.... Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto) akipongezwa na Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa baada ya kuteuliwa kuingia katika tano bora ya wawania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, kabla ya kuanza kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) katika ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma jana.

Baadhi ya Wajumbe wa kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) (NEC) wakimpongeza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kulia), baada ya kuteuliwa kuingia katika tano bora ya wawania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, kabla ya kuanza kwa kikao cha NEC, katika ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma jana.

No comments:

Post a Comment