Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday, 16 July 2015

KOMBE LA KAGAME: SIMBA SC WALIPOZIMIWA TAA NA KUPIGWA SUDAN, MALAWI IKAJITOA CECAFA 1994

 
Kikosi cha Yanga cha mwaka 1994. Waliosimama kutoka kushoto ni Salum Kabunda 'Ninja', Constantine Kimanda, Steven 'Abdulmalik' Casmir Nemes, Kenneth Mkapa, na Selemani Mkati. Waliochuchumaa ni Nico Bambaga 'Machine', Sekilojo Chambua, Edibily Lunyamila, James Tungaraza 'Boli Zozo', na Said Nassoro Mwamba 'Kizota'.


Na Daniel Mbega wa www.brotherdanny.com
HAKUNA michuano ya KLabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati iliyokuwa na mizengwe na upendeleo wa wazi kama ya mwaka 1994. CECAFA ilifumbia macho mambo maovu kabisa kwenye kandanda, ikiwabeba wenyeji kwa mbeleko ya chuma hadi kufanikisha azma yao.
Mtandao wa www.brotherdanny.com unaendelea kuwaletea uchambuzi wa kihistoria katika mashindano haya wakati tukielekea kwenye michuano ya mwaka huu ambayo itaanza Jumamosi hii jijini Dar es Salaam.
Kwanza kabisa Silver Strikers ya Lilongwe, Malawi iliwasili siku chache kabla ya mashindano lakini ilikataliwa na Katibu Mkuu wa CECAFA James Tirop wa Kenya kwa maelezo kwamba ilichelewa kujiandikisha;
Gor Mahia ya Kenya ilichelewa kuwasili katika mechi ya ufunguzi dhidi ya El Merreikh, lakini haikuadhibiwa;
Kwa hiyo Silver Strikers ilibakia mjini Khartoum kwa siku chache kwa matumaini ya kuruhusiwa kushiriki bila mafanikio, hatimaye ikarejea kwao ikiwa imepoteza gharama nyingi.
Kutokana na hali hiyo ya ubabashaji, Malawi ilijitoa CECAFA, ikifuatia hatua ya awali ya Zambia na Zimbabwe, na hazikurejea tena, badala yake zikajiunga na Shirikisho la Soka Kusini mwa Afrika (COSAFA).
Michuano ya mwaka 1994 ilifanyika katika miji ya Khartoum na Port Sudan. Kundi A lililokuwa mjini Khartoum lilizishirikisha timu za El-Merreikh (Sudan), Simba (Tanzania), Express (Uganda) na Gor Mahia (Kenya).
Kundi B la mjini Port Sudan lilikuwa na mabingwa watetezi, Yanga (Tanzania), El-Hilal Port Sudan, Electric (Ethiopia) na Shangani (Zanzibar).
Michuano hiyo iliyoanza Januari 8 na kumalizika Januari 20 iliingia dosari Januari 14 wakati Simba, ikiwa inaongoza kwa mabao 2-1 dhidi ya El-Merreikh, ilizimiwa taa uwanjani na wachezaji wake kupigwa na mashabiki, ambapo kiungo Nico Kiondo alichomwa kisu.
Simba, ambayo ilikuwa inaongoza katika kundi A, iliamua kujitoa mashindanoni na ilikuwa inazishauri timu nyingine za Tanzania, Yanga na Shangani zijitoe. Hata hivyo, timu hizo mbili hazikujitoa.
Kwa hali hiyo, El-Merreikh iliyokuwa inashika nafasi ya pili kwenye kundi hilo, sasa ilipangiwa kucheza na mshindi wa pili wa kundi B, El-Hilal. Lakini katika hatua ya kushangaza, El-Hilal iligoma kucheza na El-Merreikh kwa madai kwamba hiyo haikuwa timu ambayo ilipaswa kupambana nayo na hivyo Shangani iliyoshika nafasi ya tatu kwenye kundi B ikapambana na El-Merreikh katika nusu fainali, ambapo ilifungwa bao 1-0.
Yanga nayo ilibidi ipambane na Express waliokuwa washindi wa tatu kwenye kundi A. Katika mchezo wa nusu fainali, Yanga ilitolewa na timu hiyo ya Uganda kwa penati 5-4 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 hadi muda wa ziada, hivyo ikawa imeutema ubingwa huo iliouchukua nchini Uganda mwaka 1993. Katika kutafuta mshindi wa tatu, Yanga iliifunga Shangani mabao 2-1.
El-Merreikh ndiyo iliyotwaa ubingwa huo kwa kuifunga Express mabao 2-1 kwenye fainali.
Kwa kweli michuano hiyo ilikuwa na dosari kubwa, kwani tangu awali ilionekana wazi kwamba Wasudani walikuwa wanapendelewa na wala CECAFA haikuweza kuchukua hatua zozote za tahadhari hata pale wachezaji wa Simba walipofanyiwa fujo.

Hebu tuangalie namna mashindano hayo yalivyokwenda:
08/01/1994:- Shangani 0 vs El-Hila 1
09/01/1994:- Yanga 0 vs Electric 0
09/01/1994:- Simba 1 vs Express 2
09/01/1994:- El-Merreikh 1 vs Gor Mahia 1
11/01/1994:- Shangani 2 vs Electric 1
11/01/1994:- Express 1 vs El-Merreikh 2
12/01/1994:- Yanga 1 vs El-Hilal 1 (Fumo Felician/Amir Moussa)
12/01/1994:- Simba 1 vs Gor Mahia 0
14/01/1994:- *Simba 2 vs El-Merreikh 1 (Ramadhani Lenny, Nteze John/?) - mchezo ulivunjika dakika ya 88).
14/01/1994:- Yanga 2 vs Shangani 1
14/01/1994:- Express 1 vs Gor Mahia 0
14/01/1994:- El-Hilal 0 vs Electric 0

Kundi A
 1.El Merreikh     3  2  1  0  3- 2  5  [Sudan]
 2.Express FC      3  2  0  1  4- 3  4  [Uganda]
 3.Simba SC        3  1  0  2  3- 2  2  [Tanzania]
 4.Gor Mahia       3  0  1  2  1- 4  1  [Kenya]
   [NB: bila mabao ambayo El Merreikh iliyopewa dhidi ya Simba]

Kundi B
 1.Young Africans  3  1  2  0  3- 1  4  [Tanzania]
 2.El Hilal        3  1  2  0  2- 1  4  [Sudan]
 3.Small Simba     3  1  0  2  2- 3  2  [Zanzibar]
 4.Mebrat Hail     3  0  2  1  0- 2  2  [Ethiopia] [aka EELPA]

NUSU FAINALI:
17/01/1994:- El-Merreikh 1 vs Shangani 0 (Zahir Abdulghani 90)
18/01/1994:- Yanga 1 (4) vs Express 1 (5) (Constantine Kimanda 14, pen: Stephen Mussa, Kenneth Mkapa, Tungaraza, Mohammed Hussein/ Robert Aloro 52, pen: )

MSHINDI WA TATU:
20/01/1994:- Yanga 2 vs Shangani 1

FAINALI:
20/01/1994:- El-Merreikh 2 vs Express 1 (Fattah Rahman Santo (mawili)/Issa Sekatawa).
  [kadi nyekundu katika kipindi cha pili: Fatah El Rahman Faraq (Merreikh) na Abdul Nsubuga (Express)]

KUMBUKUMBU HIZI ZIMEANDALIWA NA MTANDAO WA www.brotherdanny.com. Tafadhali ukirejea weka chanzo cha habari.


No comments:

Post a Comment