Kikosi makini cha Yanga. Waliosimama kutoka kushoto ni Charles Boniface Mkwasa, Dotto Rutta Mokili, Hamisi Ramadhan Kinye, Joseph Fungo, Ahmad Amasha 'Mathematician', Abeid Mziba, Edgar Fongo na Muhidin Mohammed Cheupe. Waliochuchumaa ni Lawrence Mwalusako, Athumani Juma Chama, Isihaka Hassan 'Chukwu', Omar Hussein 'Keegan', Juma Mkambi, Allan Shomari, Mohammed Yahya 'Tostao', Abubakar Salum. (Naomba mnisahihishe jamani).
Na Daniel Mbega wa www.brotherdanny.com
Mashindano ya
Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame, mwaka huu
yanafanyika jijini Dar es Salaam. Blogu ya www.brotherdanny.com
inakuletea mfululizo wa dondoo mbalimbali za kihistoria kuhusu michuano hiyo
tangu mwaka 1974 ilipoanza.
Leo tunaangalia
jinsi Yanga ilivyoukosa ubingwa huo jijini Dar es Salaam baada ya kutolewa kwa
penati kwenye fainali na mabingwa wa Sudan El Merreikh mwaka 1986.
Mwaka 1986
mashindano hayo yalianza rasmi Januari 11 katika miji ya Dar es Salaam na
Mwanza hapa Tanzania yakishirikisha jumla ya timu 10. Tanzania Bara kama
mwenyeji wa mashindano hayo, iliingiza timu mbili, ambazo zilikuwa Yanga
(mabingwa wa Tanzania Bara) na Majimaji waliokuwa washindi wa pili. Timu
nyingine zilikuwa Small Simba (Zanzibar), Silver Strikers (Malawi), Wagad
(Somalia), AFC Leopards (Kenya), El-Merreikh (Sudan), Mufulira Wanderers
(Zambia), KCC (Uganda) na mabingwa watetezi, Gor Mahia pia ya Kenya.
Timu hizo zilikuwa
zimepangwa katika makundi mawili; kundi A lilikuwa mjini Dar es Salaam na timu
za Yanga, Small Simba, Leopards, KCC na Silver Strikers, na kundi B lilikuwa
Mwanza na timu za Wagad, Majimaji, Gor Mahia, Mufulira Wanderers na
El-Merreikh.
Yanga ilitolewa katika
mchezo wa fainali na El-Merreikh kwa penati 4-2 baada ya kutoka sare ya mabao 2-2
hadi muda wa nyongeza. Hadi kufikia fainali, Yanga iliifunga KCC bao 1-0 Januari
11, ikaifunga Small Simba 2-1 Januari 13, ikafungwa na Leopards bao 1-0 Januari
16 kabla ya kutoka sare na Silver Strikers.
Kwenye nusu
fainali, Yanga iliifunga Mufulira Wanderers kwa penati 4-2 baada ya kutoka
suluhu hata katika muda wa nyongeza kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
El Merreikh
ilishika nafasi ya pili kwenye Kundi B nyuma ya Mufulira Wanderers. Katika mechi
zake, Mereikh ilitoka suluhu na Mufulira, ikaifunga Maji Maji bao 1-0, ikatoka
sare ya bao 1-1 na Gor Mahia kabla ya kuichabanga Wagad kwa mabao 5-1.
Katika nusu
fainali, Merreikh iliichapa AFC Leopards bao 1-0 katika muda wa dakika 120. Hata
hivyo, Leopards ilishika nafasi ya tatu baada ya kuifunga Mufulira bao 1-0.
Katika mchezo wa
fainali dhidi ya El-Merreikh, Yanga ilibidi ijilaumu yenyewe kwa kushindwa
kuyalinda mabao yake mawili ambayo yalifungwa na Aboubakar Salum 'Sure Boy'. El-Merreikh
ilisawazisha mabao yote kupitia kwa Issa Sabah El-Kier na Ibrahim Mohammed.
Kama ulikuwa
hujui tu ni kwamba, mashindano haya ndiyo yaliyomfanya Abubakar Salum akaitwa ‘Sure
Boy’ kutokana na umahiri aliouonyesha.
Kwa upande wa penati,
wachezaji Aboubakar Salum na Charles Boniface Mkwasa waliipatia Yanga penati
mbili na Adil Amin, Kamal Abdelghani, Hamid Breima (kipa) na Atif Fadel Almoula
waliifungia El-Merreikh. Lawrence Mwalusako na Muhidin Mohammed Cheupe walikosa
penati za Yanga na Gamal Ibrahim alikosa penati kwa upande wa Merreikh baada ya
kipa Joseph Fungo kuipangua penati hiyo. Yanga hawakumalizia penati ya tano kwa
kuwa tayari walikwishatolewa. Hivyo, Wasudan wakawa mabingwa wa fainali hizo za
13.
Aidha, katika
mashindano hayo, mchezaji Aboubakar Salum wa Yanga alichaguliwa mfungaji bora
baada ya kutikisa nyavu mara nne.
Wachezaji
waliomfuatia kwa kufunga mabao matatu kila mmoja ni Gamal Ibrahim na Ibrahim
Mohammed El-Hak wote wa El-Merreikh.
Wachezaji
waliofunga mabao mawili kila mmoja ni Celestine ‘Sikinde’ Mbunga (Majimaji),
Fredrick Kashimoto (Mufulira Wanderers), Young Chimodze (Silver Strikers),
Peter Ouma (AFC Leopards), Henry Bwire Namudeche (Gor Mahia) na Adil Amin
(El-Merreikh).
Waliofunga bao moja
kila mmoja ni Mohammed Mkandinga (Majimaji), Abbas Magongo, Abbey Nassur, Benny
Oloo na Hesbone Omolo (Gor Mahia), Ali Duale na Kamal Sheikh (Wagad), Alfred
Ngwata, Ian Banda na Lewis Nhlane (Silver Strikers), Mosses Mulamba,
Wilberforce Mulamba, Michael Amwayi na Patrick Shim (AFC Leopards), Abeid Mziba,
Mohammed Yahaya ‘Tostao’, Edgar ‘Fongo’ Mwafongo, Omari Hussein ‘Keegan’ na
Dotto Rutta Mokili (Yanga), Joseph Sekitto na Charles Masiko (KCC), Hussein
Ally (Small Simba), Emmanuel Munaile, Jackson Manda, Ashtons Melu na Kennies
Mubanga (Mufulira Wanderers) na Sami Ezedin, Suleiman Makien na Issa Sabah
El-Kier (El-Merreikh).
Kundi A
AFC Leopards 2-1 Young Africans
AFC Leopards 1-1 Silver Strikers
AFC Leopards 1-0 Kampala City Council
AFC Leopards 2-0 Small Simba
Young Africans 3-1 Silver Strikers
Young Africans 1-0 Kampala City Council
Young Africans 2-1 Small Simba
Silv. Strikers 2-2 Kampala City Council
Silv. Strikers 1-0 Small Simba
Kampala CC 2-0 Small Simba
1.AFC Leopards 4
3 1 0 6-
2 7
[Kenya]
2.Young Africans 4
3 0 1 7-
4 6
[Tanzania]
3.Silver Strikers 4 1
2 1 5- 6
4 [Malawi]
4.Kampala CC 4
1 1 2 4-
4 3
[Uganda]
5.Small Simba 4
0 0 4 1-
7 0
[Zanzibar]
Kundi B
Mufulira Wand. 0-0 El Merreikh
Mufulira Wand. 2-0 Maji Maji
Mufulira Wand. 1-0 Gor Mahia
Mufulira Wand. 1-0 Wagad
El Merreikh 1-0 Maji Maji
El Merreikh 1-1 Gor Mahia
El Merreikh 5-1 Wagad
Maji Maji 1-0 Gor Mahia
Maji Maji 2-1 Wagad
Gor Mahia 3-0 Wagad
1.Mufulira Wand. 4
3 1 0 4-
0 7
[Zambia]
2.El Merreikh 4
2 2 0 7-
3 6
[Sudan]
3.Maji Maji 4
2 0 2 3-
4 4
[Tanzania]
4.Gor Mahia 4
1 1 2 4-
3 3
[Kenya]
5.Wagad 4
0 0 4
2-11 0 [Somalia]
Nusu fainali
AFC Leopards 0-1 El Merreikh [baada ya dakika 120]
Mufulira Wand. 0-0 Young Africans [baada ya dakika 120, 2-4 pen]
Mshindi wa tatu
AFC Leopards 1-0 Mufulira Wanderers
Fainali
El Merreikh 2-2 Young Africans [aet, 4-2 pen]
KUMBUKUMBU
HIZI ZIMEANDALIWA NA MTANDAO WA www.brotherdanny.com.
Ukirejea weka chanzo tafadhali cha habari.

No comments:
Post a Comment