Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday, 8 July 2015

FFU WA NGOMA AFRICA BAND WAFUNGA KAZI MAMLING FESTIVAL, AUSTRIA

 FFU kazini Mamling Festival, Austria.

 FFU wa Ngoma Africa band na gwaride la kufa mtu Mamling Festival, Austria.
 FFU wa Ngoma Africa Band wakishambulia na mitutu yao Mamling, Austria.
 FFU wakiwa Kibaruani Mamling, Festival nchini Austria.
 Kikosi kazi Ngoma Africa band kiwajibika Mamling Festival, Austria.
Mashambilizi ya FFU jukwaani Mamling Festival, Austria.

Mining, Austria
Bendi maarufu ya muziki wa dansi Ngoma Africa Band aka FFU yenye makao yake nchini Ujerumani, siku ya Jumapili 5 Julai 2015 ilifanikiwa kutingisha jukwaa la Mamling Festival,liliofanyika kule Mining, Austria.
Kikosi kazi iko cha Ngoma Africa band kilipangiwa kupanda jukwaani saa 10 na dakika 30 alhasiri,lakini maporomota walisogeza muda hadi saa 12 jioni ndio bendi hiyo ilipopanda jukwaani, muda ulisogezwa kutoka na hali jua na joto kali lililofikia nyuzi joto 38c,ambazo sio za kawaida kwa msimu summer barani ulaya.
Kikosi kazi kilipopanda jukwaani bila ya kuremba remba walianza kuporomosha muziki moto moto kama kawaida yao,kiasi cha kuwafanya waandaaji watoe mwaliko tena kwa bendi hiyo kushiriki onyesho la 2016 mungu akijalia.
Ngoma Africa baada ya kumaliza kazi wamerudi katika maskani yao ya himaya Anunnaki,kule Ujerumani

No comments:

Post a Comment