Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 5 November 2013

TMA YABORESHA HUDUMA ZA HALI YA HEWA BAHARINI NA ZIWANI


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dk. Hamza Kabelwa akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) mikakati ya Serikali katika kuendeleza huduma za hali ya hewa katika sekta ya usafiri wa baharini,Visiwani Zanzibar na katika maziwa nchini,wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo Bi. Monica Shayo.



Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Hamza Kabelwa akionesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) cheti cha utambuzi walichopokea kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Mamlaka ya Usafiri Baharini(ZMA) kutokana na kuutambua mchango wao katika usafiri wa Baharini. Kulia ni Ofisa Habari wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Georgina Misama.

MAMLAKA YA HALI YA HEWA
 
Katika jitihada za kupunguza maafa na kuhakikisha kuwa huduma za hali ya hewa nchini zinazidi kuwa bora, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imefungua kituo cha huduma za hali ya hewa kwa watumiaji wa usafiri wa baharini. Ofisi hiyo ilianzishwa rasmi tarehe 28/04/2013 katika bandari ya Zanzibar, ikiwa na lengo la kuhakikisha taarifa za hali ya hewa kwa usafiri wa baharini zinapatikana na ushauri unatokewa kwa watumiaji kwa wakati, hapo awali huduma hizi zilikuwa zinaandaliwa na kutolewa kutoka ofisi za hali ya hewa zilizopo kituo kikuu cha utabiri – Dar es Salaam na uwanja wa ndege wa Karume - Zanzibar.

Kwa upande wa usafiri katika maziwa, Mamlaka imenunua mtambo mkubwa wa kuchambua taarifa za hali ya hewa (computer cluster) utakaowezesha huduma za hali ya hewa kutolewa katika maziwa yote makuu hapa nchini.

Katika kutambua mchango mkubwa unaotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Mamlaka ya Usafiri Baharini (ZMA), iliipatia Mamlaka ya Hali ya Hewa cheti cha kuutambua mchango huo (Certificate of Appreciation) kwa kutambua mchango wa Mamlaka katika usafiri wa baharini.

Vilevile, Mamlaka kupitia ofisi ya Zanzibar ilitunikiwa cheti cha kuutambua mchango wake katika kukabiliana na maafa (Certificate of Appreciation). Cheti hicho kilitolewa na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais SMZ, Kitengo cha Maafa.
 
IMETOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA


No comments:

Post a Comment