Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 8 November 2013

NI MAAFA MVOMERO


Watu  sita wameuawa, 36 kujeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya Bwagala na 30 wanashikiliwa kufuatia mapigano na mauaji baina ya wakulima na wafugaji zilizotokea katika eneo la Hembeti wilaya Mvomero mkoani hapa huku maganda ya risasi yameokotwa katika eneo la tukio.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Faustine Shilogile, mauaji hayo yalitokea kati ya Novemba 5 na 6 mwaka huu baada ya wafugaji kuamua kuwachukulia hatua ng’ombe waliokuwa wakila mazao yao mashambani mwao.
Alimtaja mmoja kati ya waliouawa kuwa ni Yusuphu Mbutu (30), mkulima wa kijiji cha Mkindo ambaye aliuawa katika vurugu za kwanza na kwamba wengine watano wakiwamo wafugaji wa jamii ya wamasai  wawili na wakulima majina yao hayakuweza kufahamika kufuatia baadhi yao kuwa ni wakazi wa vijiji vya Wilaya ya Gairo.
Kamanda huyo alisema Novemba  jioni kundi la ng’ombe wapatao 300 mali ya mfugaji Semwako Matuna, mkazi wa kijiji cha Mpapa waliingia katika mashamba ya mpunga ya wakulima na wakulima kuamua kuwakamata na kuwafikisha katika ofisi ya kijiji cha Hembeti.
Alisema kuwa majadiliano yaliendelea  ili kuona ni namna gani wafugaji wanatakiwa kufidia gharama za mazao ya wakulima na kutakiwa kulipia kila ng’ombe mmoja Sh. 10,000 na kutakiwa kulipa Sh milioni tatu, lakini wafugaji hawakuliafiki na kutaka kuchukua mifugo kwa nguvu huku wakitumia silaha mishale, risasi za moto na marungu.
Alisema, hali hiyo ilifanya kundi la vijana wakulima kutoka Wilaya ya Gairo kujitokeza na kuanza kupambana na wafugaji na kusababisha watu tisa kujeruhiwa na mmoja kuuawa.
Kamanda Shilogile alisema wakulima hao waliamua kwenda kulipiza kisasi katika eneo la Mpapa Kibukiro na kuendelea na mapigano na wafugaji na kusababisha watu watato kuuawa huku 28 wakijeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya Bwagala.
Alisema watu 30 wanashikiliwa na polisi kufuatia vurugu hizo na kuwa maganda  ya risasi yaliokotwa eneo la tukio huku bunduki iliyotumika  mali ya mfugaji ilisalimishwa polisi.
Aliwataka wananchi walioyakimbia maeneo yao kwa kuhofia vurugu hizo kurejea kwani vurugu zimedhibitiwa. Naye Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo kutoka makao makuu ya jeshi hilo, Kamishna Paul Chagonja, aliwaasa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi bali watii sheria zilizopo bila shuruti.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment