Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 15 November 2013

BIBI KIZEE ANAYEDAIWA KUFANYA MAPENZI NA ROONEY AZUA MAMBO


Wayne Rooney (26)

MHUDUMU wa mapokezi katika jumba la upunaji (massage parlour) anayedaiwa kufanya mapenzi na Wayne Rooney alimwambia mwanandinga huyo aondoke mara moja 'kabla hajachafuliwa na soka yake kwisha', mahakama ya Old Bailey ilielezwa Jumatatu.
Patricia Tierney, 58, alikanusha kulipwa fedha ili afanye mapenzi na mwanandinga huyo katika danguro la mjini Liverpool mwaka 2004, kufuatia msururu wa taarifa kuhusu Rooney ‘kufanya mapenzi na makahaba', mahakama iliambiwa.
Mama huyo mwenye watoto saba alisema katika hati yake ya maelezo kwamba alihofia hatma ya mshambuliaji huyo wa Manchester United wakati alipomwendea kwa mara ya pili akitaka kufanya naye mapenzi baada ya kunogewa, na akamtaka aondoke haraka.
“Tukio hilo, ambalo ni la uongo, inadaiwa kwamba nilifanya mapenzi na Wayne Rooney na kwamba alinilipa katika siku isiyofahamika wakati nikifanya kazi kwenye jumba la upunaji,” alisema.
“Nakumbuka Wayne Rooney alikuja pamoja na wanaume wengine. Siku kadhaa baadaye alikuja peke yake. Safari hii nilimsukumia kwenye chumba na kumwambia avute kofia yake kuficha uso na aondoke haraka kabla hajachafuliwa na kumaliza soka yake.”
Glenn Mulcaire wa gazeti lililofungiwa la News of the World ambaye alikuwa anamchunguza Wayne Rooney wakati huo, alikutwa na jina na tarehe ya kuzaliwa ya Tierney kwenye nyaraka zake, mahakama iliambiwa.
Karatasi nyingine zilizokutwa nyumbani kwake zilionyesha kwamba jina la siri la simu ya Wayne Rooney lilikuwa Stella Artois.
Habari nyingine kwenye kompyuta iliyoandikwa 'Project Patricia Tierney' ilikutwa kwa mwandishi huyo.
“Ninaamini hii inahusiana na tukio la kwenye danguro,” alisema Tierney, akaongeza: “Nilipewa Pauni 30,000 (na News of the World) kwa ajili ya habari hiyo lakini nikakataa.”
Notebook za Mulcaire, ambaye alikuwa anaingilia mawasiliano ya siri ya Rooney, zilikubwa na taarifa zinazomhusu mama wa Rooney, mahakama iliambiwa.
Siku nyingine aliandika dokezo la taarifa za simu kuhusu mwanamitindo aitwaye Laura Rooney. Wiki iliyopita ilibainika kwamba alikuwa anamfuatilia mwanadada huyo kwa makosa akidhani kwamba ana udugu na mshambuliaji huyo wa Manchester United na England.
Mwendesha mashtaka Andrew Edis QC aliiambia mahakama: “Simu ya Laura Rooney ilitegwa na mawasiliano yake kunaswa kwa sababu walidhani ana udugu na Wayne Rooney, ambaye simu yake pia ilikuwa imetegwa ili kunasa mawasiliano yake. Hakuwa na udugu wowote na Wayne Rooney na hahusiani naye kwa lolote. Ni mtengeneza nywele ambaye hamfahamu Wayne Rooney lakini akajikuta akichunguzwa kama tu alikuwa na uhusiano naye.”
Mtendaji mkuu wa zamani wa News International Rebekah Brooks, 45, kutoka Churchill, Oxfordshire; daktari wa zamani Andy Coulson, pia mwenye miaka 45, kutoka Charing huko Kent; mkuu wa habari wa News of the World Ian Edmondson, 44, kutoka Raynes Park, kusini magharibi mwa London; na mhariri mtendaji wa zamani wa gazeti hilo Stuart Kuttner, 73, kutoka Woodford Green, Essex, wote wanashtakiwa kwa kushirikiana na wengine kuingilia mawasiliano ya simu za watu kati ya Oktoba 3, 2000 na Agosti 9, 2006.
Kesi hiyo bado inaendelea.

No comments:

Post a Comment