Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 18 November 2013

SHETANI AINGIA KANISANI

Jumapili moja asubuhi, shetani aliingia kwenye kanisa moja katika mji fulani. Kila muumini aliyekuwepo ibadani, pamoja na mchungaji na wainjilisti, wakaanza kugombea mlango wa kutokea, wakipigana vikumbo kunusuru maisha yao.
Baada ya muda kila mmoja alikuwa ametoweka kanisani, isipokuwa mzee mmoja ambaye aliketi akiwa ametulia tuli.
Shetani akamwendea na kumuuliza: "Unajua mimi ni nani?"
Mzee yule akajibu; "Yap, najua."
Shetani akauliza: "Wewe hukimbii?"
"Hapana, hakika siwezi kukukimbia," akajibu yule mzee.
Kwa mshangao, shetani akauliza: "Kwa nini huniogopi?"
Yule mzee akajibu kwa utulivu: "Nimeoa dada yako mwaka wa 48 sasa."

No comments:

Post a Comment