Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 17 November 2013

MAKABURI YA MACHIFU YANA MAMBO

Naam, kila sehemu kuna mambo yake, lakini hakuna kazi ngumu kama kuzuru makaburi ya machifu, inahitaji moyo. Hili ni kaburi la Mtwa Munyigumba Kilonge Mwamuyinga lililopo katika Kijiji cha Rungemba. 
Nilipofika hapa kwa mara ya kwanza mwili ulinisisimka mno, nikaogopa lakini nikaona fahari kubwa kwamba walau katika maisha yangu nimeweza kufika katika kaburi la Chifu Mkuu wa Wahehe, ambaye nilikuwa namsoma tu kwenye vitabu vya historia enzi hizo nikijua ni simulizi kama zilivyo nyingine. 
Kusema kwamba ipo siku ningeweza kufika hapa, au kuota kwamba kuna mahali hao mashujaa tunaweza kuona kumbukumbu zao, sikuwahi kutegemea. Hii ilikuwa miongoni mwa matukio ya kukumbukwa katika maisha yangu.
Naam, hapa pawekwe Makumbusho ya Taifa kwa sababu panaweza kusaidia kudumisha historia hii muhimu kwa vizazi vyetu. Bado naendelea na utafiti wangu.

Ndugu yenu,
Daniel Mbega
Iringa


No comments:

Post a Comment